|
Mafundi
wakiendelea na ukarabati wa meli ya MV. Clarius leo October 31,2017 katika Bandari ya Mwanza.
Kukamilika
kwa ukarabati wa Meli hiyo inayotoa huduma katika visiwa vilivyo katika ziwa
Victoria kutarudisha huduma za usafirishaji na abiria katika visiwa hivyo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
|
|
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (mbele), akitoka
kuangalia ukarabati wa meli ya Mv.
Clarius, katika Bandari ya Mwanza, leo. Meli hiyo inatoa huduma katika visiwa
vilivyo kwenye ziwa Victoria.
|
|
Muonekano wa
Meli ya Mv. Umoja yenye uwezo wa kubeba behewa 22. Meli hiyo inasafirisha
mizigo kutoka Bandari ya Mwanza kuelekea Bandari ya “Port Bell” nchini Uganda.
|
|
|
|
Mhandisi
Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Xavier Kapinga, akifafanua jambo kwa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa tatu
Kushoto mbele) wakati alipokagua maendeleo ya ukarabati wa meli katika Bandari
ya Mwanza, Leo October 31,2017.
|
|
Meneja Mkuu
wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Bw. Erick Hamissi, akimuonesha Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kulia), hatua
zilizofikiwa za ukarabati wa meli ya Mv. Clarius na Mv. Umoja katika Bandari ya
Mwanza.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amekagua eneo
lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya na yakisasa itakayotoa huduma za
usafirishaji katika Ziwa Victoria.
Akizungumza
na wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Profesa Mbarawa, amewataka
wafanyakazi wa Kampuni hiyo kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi ili kazi hiyo
ianze mara moja na kukamilika kwa wakati.
“Mkandarasi
ameshapatikana hivyo hakikisheni mnatoa ushirikiano na mnafanya uhakiki wa
kimahesabu vizuri ili kazi hii ifanyike kwa gharama nafuu, ubora na muda mfupi”,
amesema Profesa Mbarawa.
Katika hatua
nyingine, Waziri Mbarawa, amekagua maendeleo ya ukarabati wa meli ya Mv.
Clarias na Mv. Umoja ambapo ameeleza kuridhishwa kwake na hatua zilizofikiwa, na
hivyo kuwataka MSCL kutafuta mizigo ya kusafirisha kutoka Bandari ya Mwanza
kwenda Bandari ya “Port Bell”, nchini
Uganda.
“Kukamilika
kwa meli kuwiane na kasi ya kutafuta mzigo mwingi ili meli hizi zifanye biashara
wakati wote na kuhakikisha Kampuni yenu inapata mapato mengi yatakayowawezesha
kujiendesha kwa faida”, amesisitiza Waziri Mbarawa
Naye, Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Bw. Erick Hamissi, amemhakikishia
Profesa Mbarawa, kuwa wamejipanga kufanya ukarabati mkubwa wa meli za Mv.
Victoria, Butiama na Liemba ili kuziwezesha meli hizo kufanya kazi katika ubora
wake wa awali na kupunguza tatizo la usafiri katika ziwa Victoria na
Tanganyika.
“Tumeweka
mkakati wa kuhakikisha tunazikarabati meli zetu zote ili ziwe katika ubora
unaostahili wakati wote”, amefafanua Bw. Hamissi.
Katika
kuhakikisha maendeleo ya kibiashara na kuichumi
yanafikiwa katika Ukanda wa maziwa makuu
nchini, Serikali imejipanga kuhakikisha inafufua usafiri wa meli za
abiri na mizigo katika ukanda huo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
|





No comments:
Post a Comment