![]() |
|
|
![]() |
|
Kwamba Juzi,
Oktoba 29, 2017 alipokuwa kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za udiwani katika
Kata ya Kijichi, Wilayani Temeke alitoa maneno yanayoweza kupelekea uvunjifu wa
amani.
Maneno hayo ni yafuatayo:
1. Kwamba
wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kufanya uchunguzi
na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge Tundu Lissu mpaka siku hiyo.
2. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach.
Hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya
kumshambulia Tundu Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwenye fukwe.
Timu ya mawakili wa chama iko na ndugu Zitto katika mahojiano haya. Ado Shaibu - Katibu wa Itikadi, Mwasiliano ya Umma na Uenezi ACT Wazalendo Oktoba 31, 2017 Dar es salaam |







No comments:
Post a Comment