![]() |
|
HAPA CHINI ISOME TAARIFA RASMI YA
NYALANDU ALIYOITOA KUHUSU KUJIUZULU KWAKE.
NIMEAMUA
kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM,
pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017.
HALIKADHALIKA,
asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya
kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi
ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu
nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa.
AIDHA,
Nimechukua UAMZI huo kutokana na kutoridhishwa kwangu na mwenendo wa hali ya
Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za Kibinadamu, ongezeko la
vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo
kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama)
kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia
Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA.
VILEVILE,
Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya
kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na
kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na mahakama ambayo ndio
chimbuko la Uongozi Bora wa nchi, na kuonesha kwa uwazi kuwa madaraka yote
yatokana na wananchi wenyewe, na kwamba Serikali ni ya Watu kwajili ya Watu.
MIMI
Naondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia
ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa,
Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
TAIFA, kwani nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na
kiuchumi uliyopo Tanzania Sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia
Serikali kama ilivyokuwa hapo awali.
AIDHA, Naamini
kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru
kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna Moja au nyigine, CCM nayo imekuwa
Chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali
inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa TAIFA MWALIMU Julius Kambarage
Nyerere.
HIVYOBASI,
kwa dhamira yangu, na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya KIKATIBA,
natangaza KUKIHAMA Chama Cha Mapinduzi CCM leo hii, na nitaomba IKIWAPENDEZA
wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, basi waniruhusu kuingia
MALANGONI mwao, niwe mwanachama, ili kuungana na CHADEMA na watanzania wote
wanaopenda kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini kwa kupitia mfumo wa
ki demokrasia na uhuru wa mawazo.
VILEVILE, nimemua
kujiuzulu KITI Cha Ubunge, Jimbo la Singida Kaskazini kuruhusu kufanyika kwa
UCHAGUZI mwingine ili wananchi wapate fursa ya kuchagua ITIKADI wanayoona
inawafaa kwa majira na nyakati hizi zenye changamoto lukuki nchini Tanzania.
Ni
imani yangu, kamwe hayatakuwa ya bure maneno haya, wala uamuzi huu niufanyao
mbele ya Watanzania leo ili kwamba, SOTE kama TAIFA tuingie kwenye mjadala wa
kuijenga upya misingi ya nchi yetu.
|
Monday, October 30, 2017
Jibu la CHADEMA kwa Lazaro Nyalandu.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.







No comments:
Post a Comment