Update Ajali ya Gari la Tanesco Ngara-Yaua Mtu mmoja na Kujeruhi Watano. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, October 30, 2017

Update Ajali ya Gari la Tanesco Ngara-Yaua Mtu mmoja na Kujeruhi Watano.

Mtu mmoja amefariki na wengine Watano kujeruhiwa katika ajali iliyotokea jioni ya leo October 30,2017  katika eneo la Njia Panda ya kwenda Rulenge wilayani Ngara Mkoani Kagera. 

 Taarifa kutoka eneo la tukio,zinasema Ajali hiyo imehusisha  gari aina ya Canter yenye namba za usajili SU 38141 mali ya Shirika la Umeme –TANESCO wilayani Ngara.
Watu hao waliokuwa wakitumia gari hilo walikuwa wakitoka kwenye  shughuli za kikazi za kila siku.

Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya Murgwanza wilayani Ngara huku mwili wa  Mtu aliyepoteza maisha katika ajali hiyo ikihifadhiwa katika hospitali hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad