|
IGP Sirro.
Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro leo Septemba 8, 2017
amezungumza na waandishi wa habari na kueleza kuhusu matukio ya uvunjifu wa
amani yanayoendelea hapa nchini.
Sirro
amezungumzia juu ya mauaji ya Kibiti na kusema hali sasa ni tulivu na asilimia
90 ya wahalifu wameshakamatwa.
Pia
amezungumzia juu ya kauli ya jana ya Rais Magufuli kuhusu kuwakamata waliotajwa
kwa kashfa ya madini kwenye ripoti ya Biashara ya Tanzanite na Almasi na kusema
kuna watu wameshakamatwa mkoani Manyara tayari huku akieleza kuwa tukio la
watoto kutekwa Arusha kwa sasa watuhumiwa wameshakamatwa na mmoja wao
ameshauawa huku upelelezi ukiendelea.
Akizungumzia
suala la Tundu Lissu kupigwa risasi amesema wametuma wapelelezi wao wazuri
kwenda Dodoma na lazima watawakamata, akaongeza kuwa itawezekana kama wananchi
watawapa taarifa.
|
No comments:
Post a Comment