Mkuu wa
Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori (Kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati wa ziara ya kikazi katika
soko la Ndizi-Mabibo.
|
Wakuu wa
Idara na Vitengo Manispaa ya Ubungo wakifatilia mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya
Ubungo Mhe Kisare Makori uliofanyika katika Soko la Ndizi-Mabibo Jijini Dra es
salaam.
|
Wananchi
pamoja na wafanyabiashara katika soko la Ndizi-Mabibo wakifurahi mara baada ya
kuambiwa wataendelea na shughuli zao katika soko hilo.
|
Wananchi
pamoja na wafanyabiashara katika soko la Ndizi-Mabibo wakifatilia kwa makini
Mkutano.
Ziara hiyo
imejili mara baada ya uongozi wa kiwanda cha Urafiki kutaka kuwaondoa kwa nguvu
wafanyabiashara na kulifunga eneo hilo kwa kujenga uzio utakaozuia ufanyaji wa
biashara.
Mkurugenzi
amejibu hapo hapo agizo la Mkuu wa Wilaya Mhe Makori lilomtaka kusitisha mara
moja zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara hao kwa kuwaagiza Afisa Afya na
Mazingira wa Manispaa ya Ubungo kufuatilia malalamiko yaliyotolewa na wananchi
katika mkutano huo kuhusu kiwanda cha nguo cha Urafiki ambacho kinalalamikiwa
na wananchi kwa kuathiri afya zao kutokana na Moshi unaotoka kiwandani hapo.
Aidha mbele
ya umati wa wafanyabiashara na wananchi katika mkutano huo Mkurugenzi Kayombo
amemuagiza Kaimu Injinia wa Manispaa ya Ubungo kusambaza kifusi cha mawe
kilichomwagwa sokono hapo kwa ajili ya kuzuia mlundikano wa maji.
Mkurugenzi
Kayombo alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria
kukusanya mapato kwa kiasi kikubwa hivyo ameeleza dhamira yake ya kukusanya
mapato ya Zaidi ya shilingi milioni 150 kwa mwezi katika soko la Ndizi-Mabibo
na tayari mirija na mianya yote ya rushwa amefanikiwa kuiziba kwa kiasi
kikubwa.
|
No comments:
Post a Comment