Serikali
kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Utawala Bora imetangaza
kuwa watumishi wa umma 450 wameshinda rufaa, kati ya waombaji 1,050 ambao
waliwasilisha rufaa zao katika mamlaka husika baada ya kutajwa katika orodha ya
wenye vyeti feki.
Akizungumza
na wanahabari jana July 13,2017 jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Utawala Bora, Dk Laurian Ndumbaro
alisema serikali iliendesha uhakiki wa vyeti vya kidato cha nne, sita na ualimu
ambako watumishi wa umma 9,932 walikutwa na vyeti feki.
“Baada ya
kutangazwa kwa orodha hiyo ya watumishi wenye vyeti feki, watumishi 1,050
walikata rufaa na watumishi 450 pekee walishinda rufaa hizo huku watumishi
8,800 wakiridhika na matokeo hayo,” alisema Dkt Ndumbaro
“Kuna baadhi
ya walitumia majina mawili alipokuwa kidato cha nne baadae alilazimika kutumia
matatu na kubadilisha mkanganyiko hivyo tumejiridhisha na wanarudishwa katika
utumishi wa umma.”
Aidha
Ndumbaro aliongeza kuwa rufaa hizo zilizokubaliwa ni kwa watumishi wale
waliokuwa wakitumia majina ya waume zao baada ya kuolewa, ambayo yalitofautiana
na majina yaliyopo kwenye vyeti na baada ya uhakiki walionekana kama ni vyeti
feki.
Katika hatua
nyingine, Dk Ndumbaro alizungumzia suala la ajira mpya, ambapo alisema serikali
imeanza kutoa vibali vya ajira mpya kuanzia mwezi ujao, watatangaza nafasi hizo
na Watanzania wenye sifa watajaza nafasi hizo 10,184 na nyingi zikiwa kwenye
sekta ya afya na elimu.
|
No comments:
Post a Comment