![]() |
Pia
ni mwanachama kiongozi wa Umoja wa Afrika (AU) ambapo imeridhia Mkataba wa
Afrika wa Haki za Binadamu na Watu na ni miongoni mwa nchi za kwanza kabisa
Afrika kukubali kushtakiwa na wananchi wake kwa kuridhia itifaki ya Mahakama ya
Afrika ya Haki za Binadamu na pia kukubali kufanyiwa ukaguzi katika utawala
bora kupitia Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM).
"Ni
kwa sababu hizi basi tunamuasa Ndugu Lissu na wananchi kwa ujumla kujiepusha na
propaganda, kejeli na uzushi usio na msingi dhidi ya Serikali au taasisi zake
na pale ambapo wanadhani kuna haki zimekiukwa badala ya kuvunja sheria ni vyema
kutafuta haki kupitia mkondo wa kisheria ambao tumeuainisha hapo juu,"
imefafanua taarifa hiyo.
Dkt.
Abbasi amesema kuwa Serikali itaendelea kuenzi na kuilinda misingi ya
demokrasia, uhuru wa watu na kuwapa fursa wananchi kushiriki katika uchumi wa
nchi hasa wakati huu wa mageuzi makubwa ya kiutendaji chini ya Rais Dkt. John
Pombe Magufuli lakini haitavumilia mtu yeyote au kikundi chochote
kitakachojaribu kutumia uhuru wowote vibaya ili tu kukwaza azma hiyo ya Taifa.
HAPA
CHINI NIMAKUAMBATANISHIA TAMKO LA SERIKALI.
|
![](https://3.bp.blogspot.com/-8Z2xKEf8s4A/WW8ql2yZfvI/AAAAAAABENY/ejs0G4nbXsQI2Lvn3m026VftzNqUKNFtQCLcBGAs/s1600/1.jpg)
No comments:
Post a Comment