Mawakili wa
upande wa utetezi wakiongozwa na James Bwana waliiomba mahakama iwafikirie
dhamana wateja wao kwa kutumia vifungu vya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambavyo vinasema kwamba, mtuhumiwa anaonekana hana hatia mpaka pale
itakapothibitishwa na mahakama.
Upande wa
mashtaka kwa kutumia pia vifungu vya sheria ambavyo vinasema makosa ya
utakatishaji fedha hayana dhamana hivyo wakaishauri mahakama kutotoa dhamana
kwa watuhumiwa wote.
|
Upande wa
mahakama haijakubaliana na upande wa utetezi, mahakama imewanyima dhamana
watuhumiwa wote na kuiahirisha kesi hiyo hadi Julai 27, 2017.
Malinzi na
Mwesigwa walishikwa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini
(TAKUKURU) mnamo Juni 27 kwa kutuhumiwa matumizi mabaya ya madaraka waliyokuwa
nayo katika uongozi wao na kupandishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza mnamo Juni
29 na kusomewa mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya
TFF.
|
No comments:
Post a Comment