Sabas
alisema baada ya hali hiyo kutokea Askari nao kwa ujasiri walijibu na mapambano
hayo yalidumu kwa zaidi ya nusu saa ambapo Polisi walifanikiwa kuwajeruhi
wahalifu wanne kwa risasi ambao baadaye walifariki dunia wakiwa wanapelekwa
hospitali.
“Katika
tukio hilo tumefanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG na magazine mbili pamoja
na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao na hii ni dalili kuwa
tunaendelea vizuri na oparesheni yetu ambayo inashirikisha vyombo vingine vya
ulinzi na Usalama katika wilaya hizi tatu za Mkuranga, Kibiti, na Rufiji”
Alisema Sabas.
Aidha Sabas ametoa
wito kwa wahalifu wengine kuacha mara moja kufanya vitendo hivyo kwa kuwa
vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kufanya jitihada zote za kuhakikisha
kuwa maeneo hayo yanakuwa salama na wananchi wanaishi katika hali ya amani na
usalama.
Vilevile amewataka
wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana wahalifu wengine ili
kuhakikisha kuwa kila mmoja anaishi kwa usalama ambapo kwa ambaye atakayetoa
taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa wahalifu hao kiasi cha shilingi milioni
kumi kitatolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro.
Taarifa na
Jeshi la Polisi.
|
Saturday, July 01, 2017
Polisi Tanzania waua Wahalifu wanne Kibiti-Pwani.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment