Kwa muda
mrefu kumekuwepo na tuhuma mbalimbali dhidi yao kuhusu matumizi mabaya ya fedha
za Taasisi hiyo ya kitaifa na inasemekana TAKUKURU wamekuwa kwenye uchunguzi
dhidi kwa muda sasa mpaka jana walipoamua kuwatiwa nguvuni.
Hivi karibuni gazeti la Nipashe
liliandika mfululizo wa makala zilizokuwa zikielezea tuhuma za ufisadi
zilielekezwa kwa Malinzi na viongozi wenzake wa TFF.
JAMALI AMEFANYA HAYA UFISADI WA
KUTISHA TFF.
Ripoti ya ukaguzi wa fedha za udhamini wa
Kampuni ya Bia Tanzania kwa Taifa Stars iliyotolewa Oktoba 2, 2014, inaelezwa
kuwa, mbali na mambo mengine, TBL iliamua kufanya ukaguzi huo ili kujiridhisha
kama shirikisho linazingatia makubaliano yaliyomo kwenye mkataba.
Inaelezwa
katika ripoti hiyo ambayo uongozi wa juu wa TBL uliithibitishia Nipashe jana
kwamba ilifanywa na Mkaguzi Mkuu wake wa ndani, Richard Magongo, kuwa kati ya
Novemba 13, 2013 (siku 11 tangu uongozi wa sasa wa TFF uingie madarakani) na
Februari 15, 2014, Dola za Marekani 315,577 (Sh. milioni 688.368) zilitumika
bila ya nyaraka za kuthibitisha matumizi yake kinyume cha makubaliano ya
mkataba wa pande hizo mbili.
Kati ya
Novemba 11, 2013 na Machi 11, 2014, Dola za Marekani 381,248 (Sh. milioni
831.616) pia zilichotwa kwenye akaunti hiyo na kutumika kwa shughuli ambazo
hazijaanishwa katika mkataba wa TBL na TFF, ripoti inabainisha.
Mchanganuo
wa ripoti hiyo unaonesha kuwa, miongoni mwa waliotajwa kwenye ripoti hiyo
kutumia fedha hiyo ni pamoja na rais wa TFF, Jamal Malinzi, ambaye Desemba 24,
2013 alilipwa Dola za Marekani 159 kupitia vocha yenye namba 1075 zikiwa ni
gharama za malazi hotelini (Hotel accommodation).
Ripoti
inaonesha kuwa, siku hiyo hiyo (Desemba 24, 2013), Malinzi alilipwa na TFF Dola
10,000 kupitia vocha namba 1077 (Repayment to Jamal Malinzi/Marejesho ya fedha
za Jamal Malinzi), kisha Februari 6, 2014 akalipwa Dola 15,934 (Loan Repayment
to Jamal Malinzi/Marejesho ya mkopo kutoka kwa Jamal Malinzi) na baadaye
kulipwa Dola 69,471 kupitia vocha namba 1098 na Dola 63,735 kupitia vocha namba
1401.
Wengine waliopewa
fedha hiyo ya udhamini wa TBL kwa Taifa Stars ni aliyekuwa msaidizi wa Malinzi,
Juma Matandika, Ali Ruvu na mwingine aliyetajwa kwa jina la S. Madadi ambao kwa
pamoja walilipwa Dola 1,084 kupitia vocha namba 828 Februari 6, 2014.
Ripoti pia
inabainisha malipo ya Dola 3,500 Januari 16, 2014 kwa ajili ya ziara ya Katibu
Mkuu na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF jijini Nairobi.
Pia zimo
Dola 4,630 zilizochotwa Desemba 24, 2013 kugharamia mtihani wa utimamu wa mwili
kwa waamuzi (Cooper test for referees), Dola 4,120 zilizotolewa siku hiyo hiyo
kwa ajili ya Ally Mayay na Ayubu Nyenzi kufanya ziara Uganda na Dola 1,638
ambazo zilitolewa siku hiyo hiyo zikiwa fidia ya malipo ya deni la TFF kulipia
ziara ya uongozi wa shirikisho mkoani Mwanza.
Dola 4,023
zilitolewa Desemba 24, 2013 kwa ajili ya posho ya sikukuu za Krismasi na Mwaka
Mpya kwa wafanyakazi wa TFF na Dola 30,000 zilitumika kwa semina elekezi kwa
makocha iliyofanyika Lushoto (coach retreat at Lushoto), ripoti inasema.
Inaongeza:
“Dola 2,829 zilitumika kutoa rambirambi na misaada, Dola 3,298 zikakopeshwa kwa
Chama cha Soka Mbeya huku Dola 989 zikitolewa kwa Chama cha Soka Mkoa wa Mtwara
zikiwa ni msaada.”
Katika
ripoti hiyo, inaelezwa kuwa, Dola 90,000 zilitumika kulipia fidia ya kuvunjwa
kwa mkataba wa aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen na Dola 34,177
zikatumika kununua magari mawili aina ya Toyota Hiace.
Ripoti inaeleza
kuwa, kulikuwa na mawasiliano rasmi kati ya maofisa wa TFF na TBL kabla ya
kufanya malipo kwa Poulsen na ununuzi wa magari hayo.
|
Wednesday, June 28, 2017
TAKUKURU-Yawatia Mbaroni Rais wa TFF Malinzi na Katibu Wake.
Tags
# MICHEZO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
MICHEZO
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment