Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini, IGP Saimon Sirro, amefanya mabadiliko ya Kamanda wa
Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga pamoja na Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari.
Katika
mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani
Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga anaenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya, na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
(SACP) Fortunatus Musilimu.
Aidha,
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya (DCP) Dhahiri Kidavashari
amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi.
Uhamisho huo
ni wa kawaida katika kuboresha utendaji wa kazi za Polisi kwa mujibu wa kanuni,
taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
Imetolewa
na:
Barnabas D.
Mwakalukwa – ACP
Msemaji wa
Jeshi la Polisi.
Makao Makuu
ya Jeshi la Polisi.
|
No comments:
Post a Comment