“Kutokana na umakini wa askari wetu, mara tu alipofika Keko na kuomba kuwaona
ndugu zake walio mahabusu na kuwapa chakula walibaini kwamba ndani yake kuna
simu” imesema taarifa hiyo.
Haikutajwa nyama na hizo simu alikuwa anapalekewa mahabusu gani hapo gerezani.
Taarifa
zinasema kimsingi kijana huyo amevunja Kifungu cha 86 (1) cha Sheria ya
Magereza sura ya 56 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002 ambayo inakataza mtu
yeyote kuingiza magerezani kitu chochote kisichoruhusiwa.
|
Mtuhumiwa Ramadhani Nombo akiwa amebeba
mapande ya nyama ambayo yanatuhumiwa kuwa na simu tano ndani yake.
Kifungu
hicho kinatamka bayana kwamba endapo ikithibitika mtu yeyote amekamatwa na
kuingiza kitu chochote ambacho hakiruhusiwi kuingizwa gerezani, atahukumiwa
kifungo kisichozidi miezi sita (6) gerezani au faini au vyote kwa pamoja.
|
No comments:
Post a Comment