Baada ya
kuenea kwa tetesi kuwa Klabu ya Simba SC imewasilisha malalamiko ya barua kwa
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kupinga kunyang'anywa pointi 3, hatimaye
uthibitisho wapatikana.
Kitendo cha
Simba SC kuwasilisha rufaa hiyo na kuenea kwa picha ikionyesha vielelezo hivyo,
imeanza kuwakwaza mashabiki wa Yanga SC ambao walikuwa wameanza sherehe za Ubingwa
baada ya Kikosi chao kufanikiwa kutetea ubingwa wake wa VPL msimu huu ikiwa ni
mara ya tatu mfululizo tangu walipolitwaa taji hilo msimu wa 2014/2015 hadi
sasa 2016/2017.
Baadhi ya
mashabiki wa Yanga SC, wameonekana kukerwa na jambo hilo huku wakiwakejeli
Simba SC kwa kuwaita “Wazee wa pointi za mezani”.
Simba SC
imeamua kwenda FIFA kuhakikisha inapata pointi tatu ambazo kama itafanikiwa,
basi moja kwa moja itatangazwa kuwa Bingwa Ligi Kuu msimu huu 2016/2017.
Haya ni
baadhi ya maneno aliyoandika Msemaji wa Simba SC aliyefungiwa, Haji
Manara;....."Last week nilipowapongeza Yanga kwa ushindi na kuwaambia
mapambano yanaendelea,sijui kama tulielewana!! Bila shaka sasa mmenielewa, soon
tutapewa haki yetu,MWANA KULITAKA,MWANA KULIPEWA"
|
No comments:
Post a Comment