![]() |
Aaliekuwa
kocha wa Yanga SC, Mholanzi Hans Van der Pluijm amejiunga na klabu ya Singinda
United iliyopanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao wa 2017/2018.
|
![]() |
Na Pluijm
anaamua kwenda Singida United baada ya kusitishiwa mkataba wa Ukurugenzi wa
Ufundi wa Yanga wiki iliyopita.
Yanga SC ilimhamishia Pluijm kwenye Ukurugenzi wa Ufundi Novemba mwaka jana,2016 baada ya
kumleta Mzambia, George Lwandamina awe kocha Mkuu.
|
![]() |
Pluijm
amefundisha Yanga SC kwa awamu mbili tangu mwaka 2014 alipoanza kwa kufanya kazi
kwa nusu msimu, akimpokea Mholanzi mwenzake, Ernie Brandts kabla ya kwenda
Uarabuni.
Singida
United imerejea Ligi Kuu msimu huu baada ya msoto wa zaidi ya miaka 15 tangu
ishuke Daraja.
|










No comments:
Post a Comment