
![]() |
Mkuu wa Mkoa
wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga amesema idadi ya
wakimbizi waliopo mkoani humo ni ni kubwa, tofauti na uwezo wa kambi zilizopo.
Maganga
amesema hayo wakati akizungumzia uamuzi wa kuanza kuwadhibiti wakimbizi
wanaoingia Kigoma kutoka nchi za DRC, Burundi na Rwanda wanaoingia kila siku
hapa nchini.
Mkuu huyo wa
mkoa amesema kambi zilizopo Kigoma zinaweza kuhifadhi watu 150,000, lakini
waliopo sasa ni zaidi ya 300,000.
Tayari mkoa
huo umesema kuwa wastani wa kati ya Wakimbizi 500 hadi 520 kutoka DRC na
Burundi huingia mkoani Kigoma kila siku kwa ajili ya kuomba hifadhi.
Mkoa wa
Kigoma una kambi tatu za wakimbizi ambazo ni Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu,
Nduta iliyopo Kibondo na Mtendeli katika Wilaya ya Kakonko.
“Tumeunda kamati ya kuwahoji kabla ya
kukubaliwa kupata hifadhi ya ukimbizi,” amesema.
|







No comments:
Post a Comment