|
Bi.Sophia Simba.
Chama cha
Mapinduzi katika mkutano wake mkuu unaoendelea Dodoma, Nchini Tanzania,
Jumamosi ya March 11, 2017,kimemfukuza mwanachama wake mkongwe na Mwenyekiti wa
Umoja wa Wanawake (UWT) Bi.Sophia Simba.
Wakati huo
huo chama kimetoa msamaha kwa Adam
Kimbisa na kimempa onyo kali Emmanuel
Nchimbi wote ni wanachama wa CCM.
Imeelezwa
kuwa onyo kali alilopewa Nchimbi
lina maana ya kuwa hatoruhusiwa kugombea nafasi yoyote kwa kipindi cha miaka
minne.
Katika
taarifa hizo za Chama, Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida amefukuzwa pia.
Aidha baadhi ya wananchama wa CCM wamevuliwa uanachama
huku wengine wakipewa onyo kali kwa sababu mbalimbali, kubwa ikiwa ni usaliti
katika uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Kufuatia
maamuzi hayo, Sophia Simba amepoteza
rasmi nafasi yake ya Ubunge wa Viti maalumu na Uenyekiti wa UWT kwani nafasi
hizo zinahitaji mtu ambaye ni mwanachama wa chama aweze kuzishika.
Kwa hivyo,
CCM italazimika kupeleka jina jingine Tume ya Uchaguzi kuteua mbunge wa kuziba
nafasi ya Sophia, huku nafasi yake
ya Uenyekiti UWT ikisubiri uchaguzi baadae mwaka huu.
SOMA HAPA CHINI TAARIFA
RASMI.
|
No comments:
Post a Comment