|
Baadhi ya
wafadhili kutoka nchini Uingereza na
Canada kupitia kanisa la Anglikana
Dayosisi ya Kagera, wakifurahia matumizi ya fedha zao za kujenga miradi ya maji
wilayani Ngara ambapo jana walitembelea kisima cha maji cha kijiji cha
Kasharazi wilayani humo.
Picha na
habari kwa Hisani ya Shaaban Ndyamukama
|
|
Kanisa la
Anglikana dayosisi ya Kagera limejenga
visima vya maji 16 kwa mwaka 2016 katika
vijiji mbalimbali wilayani Ngara vyenye thamani ya Sh 90.6 milioni ili kuwapatia
wananchi huduma ya maji safi kuwaepusha
na magonjwa ya matumbo baada ya kutumia maji ya mito na madimbwi wilayani humo
Visima hivyo
vimefadhiliwa na Marafiki wa kanisa hilo kutoka nchini Canada na Uingereza
ambapo wananchi huchangia asilimia 20 ya
rasilimali zinazowazunguka ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu zao kujenga visima
hivyo kwa kushirikisha kamati za maji na serikali za vijiji .
Mratibu wa
mfuko wa Tumaini ulio chini ya kanisa la Anglikana wilaya ya Ngara Bw Alex Nyamkara, amebainisha
hayo jana wakati wafadhili wa kanisa hilo
walipotembelea miradi ya maji katika vijiji vya Kasharazi, Nyamahwa,
Nyakisasa, Kibirizi na Kanyinya wilayani Ngara.
Bw.Nyamkara
alisema ujenzi wa kisima kimoja
hugharimu Sh 5.64 milioni na kwamba wananchi wengi hutumia maji ya mito na madimbwi kwa
kuchanganyikana na wanyama wa aina mbali
mbali na kusababisha magonjwa ya matumbo, kuharisha na homa za vipindi kwa
watoto chini ya umri wa miaka mitano.
Alisema kata
ambazo zimenufaika na miradi ya maji kupitia kanisa hilo ni Ntobeye, Muganza
Nyamiaga, Bukiriro, Mbuba, Nyakisasa , Kibogora na Kanazi na kwamba mfuko wa
tumaini hutoa mafunzo kwa wajumbe wa kamati za
maji ili kuhifadhi vyanzo na mazingira vinapojengwa visima kwa
kukarabati miundombinu ya maji
Aidha
alisema kwa mwaka huu wameomba wafadhili
kuwaongezea fedha za kujenga visima 13 katika kata zenye mahitaji
makubwa ya maji kama Keza, Murusagamba, Rusumo,Kasulo na Kabanga ili
kuwawezesha wananchi kupata unafuu wa huduma baad ya miradi ya maji ya Benki ya
dunia kukwama kukamilika
“Tunachohimiza
wananchi ni kutunza miradi ya maji kwa kuwa ni mali yao si ya Tumaini Fund na
ikiboreshwa wanaweza kunufaika nayo kwa muda mrefu na kuwashawishi wafadhili
kuwaongezea miradi mingine” Alisema Nyamkara
Wakati huo
huo alisema wafadhili hao walitoa fedha
za kuwajengea nyumba wajane na wagane
wanaoishi na watoto yatima katika mazingira magumu ambapo na mwaka jana zilijengwa nyumba 28 zenye thamani
ya Sh 70 milioni na mwaka mwaka huu zitajengwa nyumba 17 zenyethamani ya Sh 42.5
milioni.
Hata hivyo
mmoja wa wafadhili wa kanisa hilo kutoka nchini Canada, Linda Winey
aliwahimiza wachungaji na waumini
mbalimbali katika vijiji alivyotembelea kumtumainia Mungu kwa kufanya kazi kwa
bidii wakitumia juhudi na maarifa ili
kuboresha maisha yao.
Wafadhili
hao walisema walitembelea wilaya ya Ngara katika shughuli za kiroho lakini wananchi wa
Tanzania wanakabiliwa na ugumu wa maisha hivyo kunahitajika uboreshaji
wa muiundombinu na mazingira katika
utoaji huduma bora za kijamii hasa maji, Afya, elimu na makazi kwa wasiojiweza
kiuchumi.
|





No comments:
Post a Comment