|
Bw.Nyamkara amesema kupitia wahisani hao shule 22 za kata wilayani Ngara zimenufaika
kwa kuboreshewa mazingira ya kufundishia na kujifunzia hasa kwa kujengewa
matundo ya vyoo , matanki ya maji na
miundombinu mingineyo huku wanafunzi hao wakipatiwa taa za umeme wa jua
(solar) ili kujisomea usiku.
Alisema
wanafunzi waliopatiwa baiskeli hizo hutembea umbali wa kilomita 14 kwenda na kutoka shuleni na huchelewa kuanza masomo ambapo baadhi yao
hasa wanafunzi wa kike huacha masomo kwa
kukumbana na vikwazo vya maisha wanaopata ujauzito katika umri mdogo na
kukatisha ndoto zao.
Pia lisema
shule ya sekondari ya Kabanga wanafunzi wanajengewa matundu 10 ya vyoo yenye
thamani ya Sh.42 milioni, Shule ya Sekondari Murugwanza, wanajengewa matanki ya
maji, na wanafunzi wanaofaulu kitato cha nne na cha sita ambao ni yatima
wataendelea kupewa mikopo kusomea fani mbalimbali.
“Kwa wanaojiunga na
vyuo vya uuguzi na ualimu hao wanapewa mikopo asililimia 100 na wanarudisha
baada ya kupata ajira na kuanza kujikimu pamoja na familia zao ili kuwawezesha
kutokata tamaa ya kujiendeleza kimaisha” Alisema Nyamkara
|
|
Aidha Mkuu
wa shule ya Sekondari Kabanga,Bw. Aaron Sekazoya alisema katika shule yake yenye
wanafunzi yatima 54 wanaofadhiliwa na
Tumaini fund walioko kidato cha tano na sita wanapatiwa sh 120 kwa ajili ya ada
ya mwaka na matumizi mengineyo, ikiwa ni pamoja na fedha za mitihani kwa kidato
cha nne.
Pia
wanafunzi hawa hujaza fomu maalum kwa ajili ya kutyaja mahitaji yao na hatimaye
baadhi yao hupatiwa madaftari sare za
shule na taa za kujisomea kwa wanaotoka mazingira yasiyokuwa na nishati
Alisema
shuleni kwake kunafanyika ukarabati wa
matanki mawili ya maji yenye ujazo wa lita 80,000 ili kukidhi
mahitaji ya maji shuleni ambapo kwa siku
maji yanayotumika ni kati ya lita 3,000 hadi 4,000 na kwamba shule hiyo itakuwa na wanafunzi wa bweni na kutwa 936 iwapo wataripoti wote wa kidato cha
kwanza
Wakizungumza
na wanafunzi waliopokea msaada baikeli na madaftari kwenye shule hizo marafiki wa kanisa hilo
kutoka kisiwa cha Gamsey nchini Uingereza Sofi Danford pamoja na Linda Winey wa nchini
Canada waliwataka wanafunzi kujifunza
kwa bidii na kutimiza ndoto zao kupitia taaluma ya elimu.
Linda
alisema pamoja na kuitembelea wilaya ya Ngara mkoani Kagera katika shughuli za
kichungaji, bado watahitaji kusaidia
sekta nyingine za kijamii kama kuwajengea nyumba wasiojiweza, kuelekeza
misaada kwa wanafunzi wa shule za msingi ambao baadhi yao wanakosa mahitaji
katika familia.
HABARI NA
PICHA KWA HISANI YA SHAABAN NDYAMUKAMA
|





No comments:
Post a Comment