Bandari Kavu
(ICD) ya Ruvu mkoani Pwani, ambayo ujenzi wake unalenga kupunguza msongamano wa
malori jijini Dar es Salaam, utakamilika ndani ya wiki tisa zijazo na
utagharimu Sh bilioni 7.3.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema jijini Dar es
Salaam jana kwamba ujenzi huo unafanywa na Shirika la Uchumi la Jeshi la
Kujenga Taifa (SUMA-JKT), ambao jana walisaini mkataba wa ujenzi huo na Mamlaka
ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).
Profesa
Mbarawa alisema mara tu ujenzi huo utakapokamilika, makontena yote yatapelekwa
kwenye bandari hiyo ya Ruvu kwa reli na malori yanayotoka mikoani na nchi
jirani, yatakuwa yanachukulia mizigo yao huko badala ya kuja Dar es Salaam.
“Tunatarajia
kuwa ujenzi ukikamilika ndani ya wiki hizo tisa, bandari hiyo itaanza kufanya
kazi,” alifafanua Profesa Mbarawa.
Aliongeza
kuwa kukamilika kwa ujenzi huo, kutaleta ufanisi mkubwa katika bandari ya Dar
es Salaam, kwa kuwa hakutakuwa tena na msongamano wa makontena.
Alisema ni
mpango wa serikali kwamba bandaria kavu zote za jijini Dar es Salaam, zijengwe
nje ya mji ili kupunguza msongamano wa magari.
Alisema
kujengwa kwa Ruvu ICD, kutasaidia kupunguza msongamano wa magari, kwani malori
yote ambayo kwa sasa yanalazimika kufika bandarini kwa ajili ya kuchukua
shehena mbalimbali yatakomea Ruvu.
Alisema
serikali imeamua kuwapa Suma JKT kujenga bandari hiyo, kwa kuwa wanawaamini
kwamba wataufanya ndani ya muda uliopangwa na kwa ufanisi mkubwa.
|
No comments:
Post a Comment