Dawa za
kutibu minyoo ni dawa ambazo watu wengi mtaani wanazitumia bila hata ya
kutafuta ushauri wa kitaalam. Watu wengi wakiona mtoto au mtu mzima anakula
sana moja kwa moja hufikiria sababu itakuwa ni minyoo.
Mtu akiona
anaumwa njaa sana siku hizi hufikiria tatizo litakuwa minyoo. Leo ningependa
tufahamu matumizi sahii ya dawa hizi.
Albendazole ni dawa inayotumika kutibu
watu na wanyama wanaosumbuliwa na ugonjwa wa minyoo.
Albendazole
ikitumika vizuri kama inavyotakiwa huua kabisa vimelea vyote (sensitive
parasites).
Usitumie Albendazole kama una aleji (allergy) na kiambato chochote
kilichopo kwenye albendazole au benzimidazole (mfano, Rabeprazole).
Wasiliana
na wataalam wako wa afya kama chochote kati ya hivyo viwili hapo juu
kinakuhusu.
Kabla ya Kutumia
Albendazole;
Kuna hali
mbalimbali za kiafya zinazoweza kuingiliana na albendazole. Wasiliana na
daktari wako au mfamasia kama una hali hizi zifuatazo:
• Kama ni mjamzito, unatarajia kuwa
mjamzito au unanyonyesha
• Kama una dawa nyingine yeyote ambayo
unatumia, au dawa asili au dietary supplement yeyote
• Kama una aleji(allergy) na dawa,
chakula au kitu kingine chochote
• Kama una matatizo ya ini, macho,
mifupa au kupungukiwa dawa mara kwa mara.
Zifuatazo ni
baadhi ya dawa zinazo ingiliana (interact) na albendazole :
• Cimetidine, dexamethasone au
praziquantel dawa hizi huangeza madhara (side effects) za albendazole.
• Theophylline, madhara (side effects)
ya dawa hii huongezeka endapo mtu atachanganya na albendazole.
Huu sio
muingiliano pekee unaoweza kutokea kama mtu atatumia albendazole pamoja na dawa
zingine. Upo muingiliano mwingi. Wasiliana na mtaalam wako wa afya kabla
haujaanza, haujasimamisha au kubadili dozi ya dawa yako yeyote ile.
Matumizi
Sahihi ya Albendazole
Tumia kama
ulivyoelekezwa na daktari wako. Angalia kwenye lebo ya dawa yako kwa ajili ya
maelezo zaidi.
• Tumia kwa njia ya mdomo kama
unashindwa kumeza kidonge kizima, unaweza kukitafuna kwanza kasha kumeza na
maji kidogo.
• Kama ukisahau kumeza dozi moja kwa
muda muafaka, jitahidi kunywa kabla muda haujapita zaidi. Kama muda wa kunywa
dozi nyingine umefika, endelea na dozi nyingine kama kawaida, usinywe dozi
mbili kwa mara moja. Kama umesahau kunywa zaidi ya dozi moja, wasiliana na
daktari au mfamasia wako.
• Albendazole inaweza sababisha
kizunguzungu. Madhara haya yanaweza kungezeka kama utatumia pombe na
albendazole kwa wakati mmoja.
• Albendazole inabidi zitumike kwa
uangalifu mkubwa kwa watoto wa chini ya mwaka mmoja kutokana na kuwa usalama wa
dawa hizi kwa kundi hili la watoto bado haujafhamika vizuri.
• Usitumie albendazole kama una
ujauzito au unanyonyesha. Albendazole zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa
mtoto aliyepo tumboni. Bado hakuna majibu ya moja kwa moja kama albendazole huteza
kupenya na kuingia kwenye maziwa ya mama anenyonyesha.
Na ikiwa utatumia dawa
hii na unaujauzito wasiliana na daktari wako kwa ushauri zaidi.
Nitoe wito
kwa Watanzania kuacha kutumia dawa holela bila ya kufuata ushauri wa kitaalamu.
Your Health,
My Concern
IMEANDIKWA
NA
FORD A.
CHISANZA
Pharmacist
Scientist/Researcher
at DawaCALL
Location:
Off Mandela Road, Mabibo – External,
P.o.Box:
77150, Dar Es Salaam, Tanzania.
Mobile:+255
652466430/+255 684363584
Email:
fordchisanza@gmail.com
fordchisanza@yahoo.com
|
No comments:
Post a Comment