Wachezaji wa timu ya Yanga SC wakishangilia ushindi dhidi ya timu ya Majimaji FC leo January 17, 2017 katika Uwanja wa Majimaji, Songea. |
Yanga SC wanaondoka na pointi 3 muhimu
kwa kuichapa Majimaji FC bao 1-0 katika mchezo wa Ligi
Kuu Vodacom Tanzania bara 2016/2017 kwa Bao la ushindi lililopachikwa Dakika ya
14 na Deus Kaseke.
|
Matokeo haya
yamewaweka Yanga SC kuwa Pointi 1
nyuma ya Vinara Simba SC ambao kesho
Jumatano January 18, 2017 wapo huko Jamhuri Jijini Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar.
Mechi
nyingine ambayo pia itachezwa kesho ni huko Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la
Dar es Salaam kati ya Azam FC na Mbeya City.
MSIMAMO VPL 2016/2017.
1 Simba SC Mechi 18 Pointi 44
2 Young Africans Mechi 19 Pointi 43
3 Kagera Sugar Mechi 19 Pointi 31
4 Azam FC Mechi 18 Pointi 30
5 Mtibwa Sugar Mechi 18 Pointi 30
|
No comments:
Post a Comment