Simba SC
wamebanwa mbavu katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Leo hii January 18,2017 baada ya kulazimishwa
sare ya bila kufungana na wenyeji, Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Matokeo hayo
yanayoiongezea kila timu pointi moja na yanaifanya Simba SC ifikishe pointi 45
baada ya kucheza mechi 19 na sasa wanawazidi kwa pointi mbili tu, mabingwa
watetezi, Yanga SC.
Hapo
Jana,January 17, 2017 Yanga SC, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa VPL, walicheza
Ugenini huko Uwanja wa Majimaji Jijini Sokoine na kutoka na ushindi wa Bao 1-0
dhidi ya Majimaji FC kwa Bao la mapema la Deus Kaseke .
Usiku huu,
huko Azam Complex, Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, Azam FC
watacheza na Mbeya City katika Mechi ya VPL.
|
No comments:
Post a Comment