Waziri Mkuu wa Tanzania,Mhe.Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Idara kwenye Halmashauri za Wilaya na
Manispaa wasaidie kutoa utaalamu badala ya kupingana na madiwani ili wawezeshe
kuleta Maendeleo kwa Wananchi.
Pia
amewataka madiwani wasikilize ushauri wa kitaalamu unaotolewa na Wakuu wa Idara
katika utekelezaji wa miradi iliyotengwa na Halmashauri.
Ametoa wito
huo jana mchana (Alhamisi, Januari 05, 2017) wakati akizungumza na watumishi
mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Mabada na viongozi na watendaji wa mkoa
wa Ruvuma akiwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani humo.
“Wakuu wa
Idara nyie ni washauri. Tumieni taaluma zenu kutoa ushauri, semeni bila woga
pale inapodidi. Ninawasihi waheshimiwa madiwani wasitumie fursa yao ya
‘kuazimia’ pale inapotokea kuna watumishi wenye msimamo,” alisema.
Akizungumzia
kuhsu ukusanyaji wa mapato, Waziri Mkuu alisema Serikali iko makini kwenye
matumizi kwa kila senti inayokusanywa na akawataka watumishi hao kila mmoja
aongeze mapato ya Serikali kupitia sekta aliyopo. Pia amepiga marufuku matumizi
holela ya fedha za umma.
“Kuanzia
leo, marufuku kwa fedha iliyokusanya kwa mapato ya ndani kutumika bila
utaratibu. Serikali hii haina mzaha na miradi inayotekelezwa chini ya viwango.
Mtumishi ukiharibu hapa Madaba, usidhani utahamishwa, tunamalizana na wewe
hapahapa. Wala usiombe ndugu yako akuombee uhamisho, tutakufuata hukohuko,”
alisisitiza.
Aliwataka
watumishi wa umma wote watumie Ilani ya Chaguzi ya CCM katika kutekeleza
majukumu kwani inaeleza kila kitu ambacho Serikali inatakiwa kukifanya katika
kipindi ca miaka mitano.
“Zaidi ya
hayo, ninawasihi kila Mkurugenzi atoe nakala ya hotuba ya Mheshimiwa Rais
ambayo aliitoa Novemba 20, 2015 wakati akizindua Bunge la 11, awape watendaji
wake waisome na kufanyia kazi maeneo yote aliyoyaainisha kwani ilitoa dira ya
nini anataka kufanya katika Serikali hii,” alisema.
Waziri Mkuu
alisema Serikali kwa upande wake inaendelea kuboresha maslahi ya watumishi na
imeanza kulipa madeni yaliyokuwa yamelimbikizwa.
“Serikali
imedhamiria kupunguza madeni ya watumishi na hadi kufikia Novemba 30, 2015
jumala ya sh. bilioni 28.9 zilikuwa zimekwishlipwa kwa watumishi 31,032 wenye
madai katika sekta mbalimbali. Zoezi hili linaendelea.”
Alitumia
fursa hiyo kuwakumbusha watumishi wa wilaya hiyo wajibu wao wa kuwahudumia
Watanzania bila kujali dini, itikadi, kabila au hali zao na akasisitiza kuwa
Serikali haitamuonea mtumishi yeyote ambaye anatimiza wajibu wake.
Akifafanua
kuhusu upandishaji madaraja ya watumishi, Waziri Mkuu alisema Serikali imeondoa
utaratibu wa mtumishi kulazimika kuandika barua ya kukiri kupandishwa
daraja/cheo ndipo aanze kupata stahili zake mpya.
"Hii
imeondoa ucheleweshaji wa kufanyika marekebisho ya mshahara na pili imeondoa
tofauti za mishahara kwa watumishi wenye ngazi moja (sifa sawa za kitaaluma,
tarehe moja ya kuajiriwa) ambao walikuwa wakilipwa tofauti kwa sababu mmoja
aliwahi kuandika barua ya kukiri na mwingine alichelewa kuandika barua kama
hiyo hiyo, " alisema.
IMETOLEWA NA
OFISI YA
WAZIRI MKUU
|
No comments:
Post a Comment