Nchi hiyo
yenye watu wapatao milioni 7.3 ina makabila mengi yanayotofautiana mila.
Tena
basi mengine yana mila mbaya na za kutisha na wanakiuka haki za binadamu kwa
kiasi kikubwa.
Katika mapori wanaoishi watu hao ni jambo la kawaida mtu ‘akionwa’
na wazee wa kimila kwamba ni mchawi, huteswa kwa kuchomwa na silaha zenye ncha
kali lakini baya zaidi humalizwa kwa kukatwakatwa kisha kufukiwa kwenye shimo.
Yapo
makabila mengi katika visiwa hivyo ambavyo vipo mashariki ya mbali, karibu na Indonesia na Australia. Baadhi ya
makabila yanaishi maisha duni na ya enzi ya ujima.
Kuna kabila ambalo mwanamke
akifiwa na mume, hukatwa kidole kimoja, akifiwa na mtoto, hukatwa kidole
kingine, huwa hivyo hata ukifiwa watoto watano, basi vidole vitano vitakatwa.
|
Wenyewe
wanasema hiyo ni njia ya kuomboleza eti kwamba uwe na uchungu halisia baada ya
kufiwa na ndugu yako wa damu, mtoto au mume.
Haijaelezwa kwa nini wanaokatwa
vidole huwa ni wanawake tu maana hata picha kwenye mitandao, wengi wa
waliopoteza vidole wanaoonekana ni wanawake, tena wale wazee au wakongwe!
|
Makabila
yanayofanya vitendo hivyo yameelezwa kuwa ni ya Dani na Kuru ambayo mengine
yanapatikana katika nchi ya Indonesia pia. Inaelezwa inapotokea mtu amefariki
dunia, mama mhusika huitwa na kuingizwa katika chumba maalum na kuulizwa
anataka akatwe kidole gani.
|
Akionesha,
kidole hukatwa bila sindano ya ganzi kwa pigo moja ya panga yenye makali na
kupakwa dawa za mitishamba kisha mama aliyekatwa hutoka ndani huku akilia na
ndipo waombolezaji wengine hudakia kulia kwa nguvu.
Baada ya
kidole kukatwa ncha iliyokatwa pamoja na
kucha, huchomwa moto na wazee wa kimila huku wakiimba nyimbo za makabila yao.
Mara baada
ya zoezi hilo kinachofuata na kidole kuchomwa moto na kuwa jivu kisha majivu
yake huwekwa kwenye chombo maalum na baadaye hufuata zoezi la majivu hayo
kupakwa nyuso za waombolezaji wote ambao wapo kwenye msiba huo.
|
Kwa kawaida
watu hao hawavai nguo na badala yake hutumia magome ya miti na wanaume hufunika
dhakari yao kwa aina fulani ya vibuyu.
Kuna vibuyu vina ‘mkono’, basi hutumia
mikono hiyo kuingiza kwenye dhakari na kuifunga kwa njia ya kitamaduni, lakini
sehemu nyingine za eneo hilo nyetu huachwa wazi na hupita hata mbele ya watoto
wao bila kuona haya!
Kwa upande
wa wanawake, wao hufunika nyeti zao kwa magombe ya miti na matiti yao huachwa
wazi vila kufunika chochote!
Kabila la
Kuru wao kama aliyefariki dunia alikuwa ni kiongozi, basi ubongo wake hutolewa
na kuliwa na wanaume.
|
No comments:
Post a Comment