Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya upatikanaji wa chakula nchini leo January 16,2017 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Mathew Mtigumwe. |
Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi akitoa
maelekezo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa Waziri
wa Wizara hiyo Dkt. Charles Tizeba9hayupo pichani) na waandishi hao kuhusu hali
ya upatikanaji wa chakula nchini leo jijini Dar es Salaam.
|
Baadhi ya
waandishi wa habari wakifuatilia mkutano baina yao na Waziri wa Kilimo, Mifugo
na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba (hayupo pichani) kuhusu hali ya upatikanaji wa
chakula nchini, mkutano umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo leo
jijini Dar es Salaam.
Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.
Aidha Dkt.
Tizeba aliongeza kuwa pamoja na kuwepo kwa hali nzuri ya chakula, Serikali
kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imeendelea kuweka akiba ya
chakula kwa kununua jumla ya tani 62,087.997 za mahindi ili kuhakikisha nchi
inaendelea kuwa na chakula cha kutosha.
Dkt. Tizeba
amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Serikali imejipanga kununua jumla ya tani 100,000 za
chakula ambapo hadi kufikia Januari 8
mwaka 2017 imenunua jumla ya tani 62,087.997 za mahindi sawa na asilimia 62 ya
lengo ililojiwekea.
“Kati ya kiasi
kilichonunuliwa, tani 38,162.280 zimenunuliwa kupitia vituo vya ununuzi na tani
23,925.717 kupitia vikundi vya wakulima hivyo hadi kufikia tarehe 12 Januari,
2017 Wakala wana akiba ya tani 88,152.443 za mahindi,” alisema Dkt. Tizeba.
Waziri
Tizeba ameongeza kuwa hadi kufikia katikati ya mwezi Januari, 2017 hali ya
chakula na upatikanaji wake hapa nchini bado ni ya kuridhisha na hasa
upatikanaji wa vyakula kama mchele na maharage ikilinganishwa na zao la
mahindi.
Aidha,
Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, FAO, TFNC pamoja na
wadau wengine wanaendelea kufanya tathmini ya kina ya hali ya chakula na lishe
nchini ambayo inatarajiwa kukamilika Januari 28 mwaka 2017 na itazihusisha
Halmashauri 55, tathmini hiyo itaiwezesha Serikali kupata taarifa za uhakika
zaidi kuhusu hali ya chakula na lishe nchini.
Amefafanua
kuwa kutokana na hali ya mwenendo wa unyeshaji wa mvua za vuli na msimu
kutokuridhisha katika maeneo mengi ya nchi, Serikali imewashauri wakulima
kutumia mbegu zitakazokomaa mapema na kupanda mazao yanayostahimili ukame
pamoja na kutumia kwa uangalifu na kuhifadhi akiba ya chakula cha kutosha kwa
matumizi katika kaya.
Aidha, Sekta
binafsi zimehamasishwa kuendelea kushiriki katika kutoa masoko ya kununua na
kuuza mazao katika maeneo yenye ziada na kuyauza katika maeneo yenye uhaba.
Ufafanuzi
huo umetolewa kufuatia kuwepo kwa taarifa za upotoshwaji juu ya hali ya
upatikanaji wa chakula hapa nchini ambapo Dkt. Tizeba amesema huo ni upotoshaji
wenye lengo la kuwatia hofu wananchi.
|
No comments:
Post a Comment