Rais Dkt.Magufuli ashiriki Ibada ya Jumapili ya Mwaka Mpya 2017 katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 01, 2017

Rais Dkt.Magufuli ashiriki Ibada ya Jumapili ya Mwaka Mpya 2017 katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibusu mkono wa Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini mara baada ya kuwasili katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya Ibada Leo January 01,2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea katika katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera mara baada ya kuwasili na kupokewa na Askofu  wa Jimbo Katoliki la Bukoba  Desiderius Rwoma (katikati) pamoja na Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini wa kwanza (kulia)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba  Desiderius Rwoma mara baada ya kushiriki Misa ya Mwaka mpya kanisani hapo. Katikati ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika kaburi la Marehemu Kadinali Rugambwa mara baada ya Ibada kanisani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba  Desiderius Rwoma mara baada ya Ibada.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ibada ya mwaka mpya katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera mara baada ya Ibada.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na masista kanisani hapo mara baada ya Ibada. PICHA NA IKULU.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad