![]() |
“Pendekezo
lao lilikuwa linalenga kuongeza bei ya umeme kutoka wastani wa shilingi 242.2
kwa uniti hadi shilingi 286.28 kwa uniti, sasa tumepunguza katika makundi yote
ya wateja, na tumekataa kuongeza gharama ya asilimia tano kwenye kundi la
watumiaji wa uniti chini ya 75 kwa mwezi,” alisema Ngamlagosi.
Alisema
shirika hilo lilipendekeza kupandisha gharama za umeme ili kufikia mapato ya Sh
trilioni 1.9 mwakani,2017 lakini baada ya Bodi ya Ewura kufanya uchambuzi wake
iliridhishwa na hoja hizo, lakini haikuona sababu ya kuongeza kwa asilimia
18.19, badala yake ikapunguza hadi wastani wa asilimia 8.5 sawa na mapato ya Sh
trilioni 1.6 .
Ngamlagosi
alifafanua kuwa kupanda kwa gharama hizo hakutaathiri maeneo mengi, isipokuwa
la D1 linalojumuisha wateja wa majumbani wenye matumizi ya wastani wa uniti 75
kwa mwezi.
Kwamba matumizi yatakayozidi, yatatozwa kwa bei ya juu ya Sh 350 kwa
kila uniti.
Kwa wateja
wa kundi la T1 ‘A’ linalohusisha wateja wa matumizi ya kawaida, ambao ni wa
majumbani, wafanyabiashara na taa za barabarani, kunaongezeko la asilimia 7.0
kutoka bei iliyopo sasa. Wakati kundi la T1 ‘B’ linalohusisha viwanda vidogo,
mabango, minara ya mawasiliano, imeongezeka kwa asilimia 8.4 sawa na Sh 124 kwa
uniti.
Kwa wateja
walioko katika kundi la T2 linalojumuisha wateja wenye matumizi ya kawaida ya
umeme wa volti 400 ambao matumizi yao kwa mwezi ni zaidi ya uniti 7,500 na
mahitaji ya umeme hayazidi 500 kVA kwa kipindi cha usoma mita, imeongezeka kwa
asilimia 8.8 kutoka bei ya sasa.
Wateja wa
kundi la T3 MV waliounganishwa katika msongo wa kati wa umeme, umepanda kwa
asilimia 7.5 kutoka kwa bei ya sasa huku walioko katika kundi la T3 HV
waliounganishwa katika msongo mkubwa umeongezeka kwa silimia 5.7.
Katika maombi
hayo, Tanesco ilibainisha sababu kadhaa ikiwamo kusaidia utekelezaji wa miradi
mikubwa mitatu ya upanuzi wa mitambo ya umeme, kuboresha miundombinu ikiwamo
nguzo na transfoma na mradi mwingine wa kuboresha mtandao wa kusafirisha na
kusambaza nchi nzima.
Aprili mwaka
huu,2016 Tanesco ilituma maombi kwa Ewura ya kupunguza gharama za umeme kwa
asilimia 1.1, lakini baada ya mamlaka hiyo kupitia maombi hayo, ilipunguza
gharama hizo kwa asilimia 1.5 hadi 2.4.
|







No comments:
Post a Comment