MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga
(NHIF) umefanikiwa kulipa vituoni madai yanayotokana na huduma za afya kwa
wakati zaidi ya bilioni 5.1 kwa mwaka wa fedha 2015/2016 sawa na
asilimia 148.
Malipo hayo yamesaidia huduma kuboreshwa
kwenye vituo mbalimbali ikiwemo watoa huduma kuhamasika na uelewa juu ya mfuko
huo .
Hayo yalisemwa hivi karibuni na Meneja wa
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Bw.Ally Mwakababu (Pichani
)wakati akitoa taarifa ya utendaji wa mfuko huo kwa waandishi wa habari mkoani
hapa.
Ambapo alisema kwenye kipindi cha mwaka
2014/2015 walilipa kiasi cha zaidi ya bilioni 3.5 hali inaonyesha ongezeko kwa
mwaka huu.
Alisema pamoja na malipo kuongezeka lakini
bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo huduma za afya vijijini
imekuwa kikwazo sanjari na upatikanaji wa dawa vituoni.
Aidha alisema lakini pia kuongezeka kwa
magonjwa yakiwemo ya ukimwi ikiwemo upungufu wa watumishi katika sekta ya afya.
“Lakini changamoto nyengine ni ugonjwa
wa ukimwi kwa wanachama ni chanzo cha magonjwa nyemelezi na lakini pia
halmashauri hazijachangamkia mikopo ,vifaa tiba,ukarabati na dawa kwenye vituo
vyao “Alisema.
Aidha alisema katika kuhakikisha uhai wa mfuko
huo unakuwa endelevu mfuko huo uliamua kufanya ukaguzi kwenye vituo
vinavyoashiria wizi na udanyanifu.
“Katika kipindi hicho mfuko umefanikiwa kuokoa
kiasi cha zaidi ya milioni 83.6 kutokana na ukaguzi maalumu 29 zilifanyika
kwenye vituo 22 kutokana na kuona vinaashiria vya hujuma au uadanyanyifu wa
huduma kwa wanachama wa Bima ya Afya “Alisema.
“Kaguzi hizo zilifanyika kwenye vituo
vya serikali 10 sawa asilimia 45,vituo vya madhehebu ya dini 8 sawa na asilimia
36 na vituo vya watu binafsi 4 sawa na asilimia 19 “Alisema.
|
No comments:
Post a Comment