Picha juu na chini, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika benchi la
kibanda cha kupigia kiwi (Shoe Shine) pamoja na wakazi wengine wa Chato katika
eneo maarufu kama Stendi za zamani Chato mkoani Geita.
Kibanda hicho cha Kiwi
ndicho Rais Dkt. Magufuli alichokuwa akisafishiwa viatu vyake kabla ya kuwa Rais, pia ni sehemu
ambayo alikuwa akipenda kukaa na
kubadilishana mawazo na wakazi wa Chato wakati akiwa mapumzikoni kipindi
cha Nyuma.
|
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 9 Januari,
2017 amefanya ziara ya kushtukiza katika Shule ya Msingi Chato,ambapo ndipo
aliposoma kuanzia darasa la kwanza hadi la saba na kuzungumza na walimu na
wanafunzi wa shule hiyo.
Rais Dkt
Magufuli ameahidi kujenga madarasa matatu na ofisi moja ya walimu katika Shule
hiyo kufuatia ombi la Walimu kuwa shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya
madarasa ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi wanaosoma shuleni hapo.
Aidha
Dkt.Magufuli amewaasa wanafunzi kutilia mkazo masomo ili waweze kufaulu na
kuwataka walimu kuhakikisha wanatumia vyema fedha zinazotolewa na Serikali kila
mwezi katika kutoa elimu bila malipo na pasiwe na wanafunzi hewa kama ilivyo
kwa baadhi ya shule ambazo zimegundulika kuwa na wanafunzi hewa katika uhakiki
uliofanywa na serikali.
Kwa upande
wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chato, Bwana Mwita Chacha amemshukuru Rais
Dkt.Magufuli kwa msaada aliowapatia katika kukabiliana na uhaba wa madarasa
uliokuwa unaikumba shule hiyo, pia kuitembelea Shule yao jambo ambalo limewatia
moyo walimu na wanafunzi shuleni hapo.
Rais
Magufuli pia ametembelea eneo la Stand ya zamani na kuzungumza na baadhi ya
wananchi waliokuwepo eneo hilo na kutoa msaada kwa kikundi cha wasafisha viatu
ili kuongeza mtaji wa biashara yao.
Jaffar Haniu
Naibu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato,
Geita.
9 Januari,
2017
|
No comments:
Post a Comment