Ikumbukwe ,Yanga
SC baada ya kusukumwa goli 4-0 na Azam
FC kwenye mchezo wa January 07,2017, wakajikuta wanamaliza katika nafasi ya
pili kwa pointi zao 6 nyuma ya Azam FC yenye pointi 7.
Kwa mujibu
wa kanuni za mashindano, kinara wa kundi A anakutana na mshindi wa pili kutoka
Kundi B wakati Kinara wa Kundi B yeye anakutana na timu iliyoshika nafasi ya
pili katika Kundi A na hapo ndipo mechi ya Simba SC na Yanga SC inapozaliwa.
Hii ni mechi ya tano kwa watani wa jadi kwenye
uwanja huo.
|
Taifa
Jang’ombe ndio timu pekee kutoka Zanzibar ambayo imefuzu hatua ya nusu fainali
ya kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2017.
Taifa
imefuzu baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya URA ya Uganda ambao ndio walikuwa
mabingwa watetezi wa taji hilo.
Bao la Mohamed Said ‘Messi wa Unguja’
limeifanya Taifa ifikishe pointi tisa pointi moja nyuma ya Simba ambao ni
vinara wa Kundi A.
|
Mechi 2 fainali ya kombe la Kagame ambapo
mwaka 1975 Yanga SC ilishinda 2-0, mwaka 1992 Simba SC ilishinda kwa
penalti baada ya kutoka sare 1-1 .
Simba SC ilishinda mechi ya ligi kuu 1-0 na
fainali ya kombe la mapinduzi 2-0.
Mechi hizo nne zinaonyesha Simba SC ikiwa na Historia ya kuifunga Yanga SC mara nyingi katika Uwanaja wa Amani. Hivyo basi tusubiri mchezo huo utakavyopigwa je Simba SC Historia itambeba au Yanga SC ndio itakuwa inafuta uteja ndani ya uwanj huu wa Amani. |
No comments:
Post a Comment