Mkuu wa
Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akizungumza kuhusu juhudi ambazo
zinafanywa na taasisi hiyo kwa ajili ya kusaidia jamii na malengo ya kutoa
msaada katika Hospitali ya Sekou Toure.
“Tunafahamu
kwamba asilimia 32 ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano vinatokea katika
siku 28 za mwanzo lakini pia tunaelezwa kuwa kila mwaka cha wanawake 8,000
hufariki dunia wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua kwa sababu ambazo
zinaweza kuzuilika na sisi kitu cha kwanza tunachotaka ni kusaidia mapambano ya
kupunguza vifo vya watoto na wanawake,” amesema Barbara.
Nae mgeni
rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ameitaja Taasisi
ya MO Dewji kuwa mfano wa kuigwa kwa msaada ambao wameutoa kwa hospitali ya
mkoa huo na kuwaomba kuendelea kuwasaidia pindi wanapohitaji msaada zaidi.
|
Mgeni rasmi
katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akizungumzia mipango ya
Serikali kuboresha huduma za afya lakini pia kuishukuru Taasisi ya MO Dewji kwa
msaada ambao wamewapatia.
“Ukimpa mama
afya bora, umesaidia jamii nzima, jambo lililofanywa na Taasisi ya MO Dewji ni
kubwa sana, hospitali zetu zinamahitaji makubwa sana na kwa hili ambalo
wamefanya ni mfano wa kuigwa na watu wengine, tunawashukuru sana na tunawaomba
muwe tayari kutusaidia kwa muda mwingine,” amesema Mongella.
Kwa upande
wa Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kemirembe Lwota amesema aliomba Taasisi ya MO
Dewji kuwasaidia baada ya kuona changaoto nyingi ambazo zinawakabili wanawake
ambao wanakwenda kujifungua katika Hospitali ya Sekou Toure na watoto ambao
wanazaliwa.
|
Mbunge wa
Viti Maalum (CCM), Kemirembe Lwota akieleza sababu ya kuiomba msaada Taasisi ya
MO Dewji ili iwasaidie vitanda, magodoro na mashuka kwa ajili ya wodi ya
wazazi.
“Rais
Magufuli alikuja hapa na hata yeye aliona changamoto ambazo zinatukabili na
mimi kama mbunge niliamua kwenda kuzungumza na watu wa MO Dewji Foundation na
napenda kuwashukuru kwa kukubali kutusaidia na naamini msaada huu utasaidia
kupunguza baadhi ya changamoto ambazo zilikuwa zinatukabili,” alisema Lwota.
|
Mganga Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Leonard Subi akitoa taarifa ya Hospitali ya Sekou Toure.
Nae Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Leonard Subi amesema hospitali hiyo licha ya
changamoto ambazo zinawakabili inahudumia wagonjwa 500 kwa siku na kwa wanawake
ambao wanafika kujifungua kwa siku wanakadiriwa kuwa kati ya 30 na 40.
|
Mmoja wa
wanawake ambao wamejifungua katika Hospitali ya Sekou Toure, Eveline Francis
akiishukuru MO Dewji Foundation kwa msaada ambao wametoa kwenye hospitali hiyo.
|
No comments:
Post a Comment