Uwanja wa Kaitaba –Bukoba/Kagera.
Ligi Taifa
daraja la 3 mkoani Kagera imeendelea leo,Ijumaa January 20,2017 kwa michezo miwili kuchezwa saa nane
mchana na saa 10 jioni katika uwanja wa Kaitaba ambapo Kagera United kucheza
na Halmashauri Misenyi huku Mabingwa watetezi Murusagamba FC ya Ngara kucheza na Kombora
FC ya Muleba.
Matokeo ya
mchezo wa Kwanza –kwa mujibu wa Katibu mkuu wa chama cha Soka mkoani Kagera -KRFA- Salum
Umande Chama- Kagera United waeshinda
mabao 3-0 dhidi ya Halmashauri Misenyi huku Murusagamba FC wakijiimarisha
kuutetea Ubingwa wao kwa kucheza Mtu 9 tu kwa Kuwafunga Kombora FC mabao 11-1.
Mpaka sasa
kundi A timu zilizofuzu kwenda hatua ya Robo fainali kutoka kituo hicho ni
Majengo FC na Muleba Stars walkimaliza mechi zao za kundi huku Kundi B- Timu ya Kagera United ikitangulia
kufuzu kwa kufikisha alama 10 huku akiwasubiri kati ya Murusagamba FC wenye
alama 7 au Vatican City wenye alama 6 ambapo wataamuana nani aungane na Kagera
United hapo january 22,mwaka huu watakapocheza mchezo wao wa mwisho wa Kundi hilo.
Timu hizo
zitaanza hatua ya robo fainali January
24,2017 kwa mshindi wa kwanza kundi A kucheza na mshindi wa pili kundi B huku
robo fainali ya pili ikipigwa january 25 kwa mshindi wa kwanza kundi B kucheza
na Mshindi wa kwanza kundi A.
Tayari
Makamu Bingwa wa msimu uliopita ,Nzaza FC ya wilayani Ngara na Eleven Stars ya
Misenyi zimefuzu kutoka kituo cha Karagwe na sasa wanawasubiri washindi wawili
watakao fuzu kutoka kituo cha Bukoba ili kucheza Ligi itakayotoa Bingwa wa Mkoa
wa Kagera wa Ligi hiyo kwa Msimu huu.
|
No comments:
Post a Comment