Mapera ni
matunda ya msimu yenye wingi wa vitamini A na C, madini ya potasiam, nyuzi
nzuri ya fiber na ‘lycophene’ vyote hivi ni muhimu kwa afya ya binadamu.
Watu wengi
hutumia tunda tu bila kujua kuwa si tunda pekee lenye manufaa kwa afya. Majani
ya mpera ni mazuri kwa ajili ya ngozi, nywele na afya kwa ujumla, leo tuangazie
faida ya majani hayo kwa afya ya binadamu kwa kuyanywa kama chai.
Namna ya
kuitengeza chai ya majani ya mpera ni rahisi. Kuna namna mbili, kwanza kwa
kuchemsha maji kama glasi nne mpaka itokote sana, chukua majani kama 10 ya
mpera, weka ndani ya yale maji moto alafu funika kwa dakika 10 – 15.
Koroga
chuja, weka kwenye kikombe, hapo chai itakuwa tayari kwa kuinywa.
Aina
ya pili ni chemsha maji hayo pamoja na majani kama kumi yakiwa ndani,
yachemke kwa dakika 10 -15, chuja tia asali badala ya sukari, chai
tayari. Waweza kutumia majani ya mpera yaliyokaushwa pia.
Unaweza
kutumia majani ya mapera kama chai na utapata faida 18 zifuatazo:
1.’Chai’ ya
majani ya mpera inasaidia mwili kuwa stadi, inasaidia madini ya carbohydrates
yasigeuzwe kuwa sukari ndani ya mwili hivyo kupunguza hamu ya kula.
2.Chai ya
majani ya mpera pia inashusha kiwango cha sukari mwilini na kuzuia mwili
kuondoa ‘insulin’. Kwa sababu hii, wagonjwa wa sukari wanashauriwa kuitumia
mara kwa mara.
3.Chai ya
majani ya mpera pia hupunguza lehemu mbaya (bad cholestrol) bila kudhuru lehemu
nzuri.
4.Chai hii
ina nguvu za kudhibiti vijidudu vya magonjwa mwilini hasa kuzuia magonjwa ya
kuharisha na kipindupindu.
5.Chai hii
inatibu mchafuko wa tumbo na pia inasaidia kukabili madhara yaletwayo na
chakula chenye sumu.
|
No comments:
Post a Comment