Ule wimbo
unaosikika mtaani wa ‘pesa kupotea mifukoni’ haumhusu Bosi wa WCB, Diamond
Platinumz anayeendelea kuzihesabu ‘deals’ kubwa zaidi za matukio ambayo dunia
nzima inayaangalia kwa macho yote.
Siku chache
baada ya kutumbuiza kwa ustadi mkubwa kwenye tuzo za CAF jijini Abuja nchini
Nigeria, Diamond amealikwa kutumbuiza kwenye ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya
Africa 2017 (AFCON 2017), Januari 14,2017 nchini Gabon.
Chibu
Dangote amewapa habari hiyo njema mashabiki wake kupitia mitandao ya twitter na
Instagram, kwa kupost taarifa ya show yake hiyo iliyowekwa kwenye akaunti
maalum ya AFCON 2017.
“GABON!!!
You know we gat to make a World History on the 14th January right?? See you
this this Coming Weekend then…👈
#WcbWasafi” aliandika.
Ingawa
Tanzania haipo miongoni mwa nchi zinazoshiriki kombe hilo kubwa zaidi la soka
barani Afrika, mwaka huu bendera itapeperushwa kupitia tasnia ya Muziki na
kuiacha alama ya Tanzania kwenye mashindano hayo.
|
No comments:
Post a Comment