
![]() |
Imedaiwa
kuwa baada ya kufika Dar es Salaam, aligundua kuwa amesahau kuchukua kadi ya
bima ya afya, na hivyo akalazimika kurudi Iramba.
Jana asubuhi
Janet alichelewa basi la National Express katika kituo cha Kyengenge na kuamua
kukodi bodaboda kulifukuzia basi hilo na kufanikiwa kulikuta kituo cha Malunga.
Baada kupanda basi hilo, dakika chake baadae, basi hilo lilipata ajali na
kulaliwa na basi kichwani.
Watu hao
wamefariki dunia papo hapo na miili yao ipo katika chumba cha kuhifadhia maiti
cha hospitali ya mkoa mjini Singida.
Basi hilo lilikuwa linatokea Kiomboi,
likielekea jijini Dar.
|
![]() |
Akizungumza
kwenye eneo la tukio, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida , ACP Debora
Daudi Magiligimba, alisema ajali hiyo imetokea Desemba, 30 saa 12.45 asubuhi
katika eneo la kijiji cha Tumuli.
Alisema
ajali hiyo pia imesababisha majeruhi 26 ambao wamelazwa katika hosipitali ya
mkoa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Kamanda
Magiligimba alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa ajali hiyo kwa kiwango
kikubwa imesababishwa na mwendo kasi na uzembe.
“Eneo hili
ilipotokea ajali hii kuna mteremko na kona kali. Kutokana na mwendo kasi,
dereva alishindwa kulimudu na hivyo kuacha barabara na kuingia kwenye korogo la
mto, na kuruka juu kisha kupinduka mara tatu,” alisema.
Kwa upande
wake mganga mkuu mkoa wa Singida, Dk. John Mwombeki, alikiri kupokea miili ya
watu wawili waliofariki dunia kwenye ajali ya basi la National Express, pamoja
na majeruhi 26.
|
![]() |
“Kati ya
majeruhi hawa, mmoja dada Joyce tumempa rufaa kwenda hospitali ya taifa
Muhimbili kutokana na sehemu yake ya mwili ya chini kutokufanya kazi. Majeruhi
10 wao tunaendelea kuwafanyia uchunguzi” alisema Dk. Mwombeki.
Mmoja wa
majeruhi hao mfanyakazi wa shirika la TBC jijini Dar es Salaam, Victor Elia,
alisema pamoja na kupoteza kila kitu, anamshukuru Mungu kwa kupona kufa kwenye
ajali hiyo mbaya.
“Kilichonisaidia
ni kufunga mkanda … abiria wenzangu wote ambao hawakufunga mikanda ndio
walioumia zaidi wakiwemo waliopoteza maisha. Ajali hii kwa vyovyote imechangiwa
na mwendo kasi,” alisema Victor ambaye ni mtayarishaji na mtangazaji wa TBC.
Kondakta wa
basi hiyo, Nicolaus Apolinari (23) mkazi wa jijini Dar es Salaam, alisema ajali
hiyo imechangiwa na utelezi uliosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katika
eneo hilo.
![]() ![]() |
No comments:
Post a Comment