Jeneza lenye
mwili wa aliyekuwa kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba
ukitolewa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya VETA mjini hapa kwa ajili
ya kuagwa na viongozi mbalimbali na wananchi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa
Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe. Baada ya kuagwa kwa mwili huo
umesafirishwa hadi kijiji cha Kawajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi.
|
Jeneza lenye
mwili wa aliyekuwa Kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba
ukitolewa kwenye basi dogo lililobeba mwili huo kutoka hospitali ya taifa
Muhimbili jijini Dar-es-salaam. Mwili huo umefikishwa kwenye nyumba aliyokuwa
akiishi mjini Singida kwa ajili ya kuagwa leo (01/12/2016).
|
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akiwashukuru wananchi
waliojitokeza kwa wigni kuungana na familia kwa ajili ya kuaga mwili wa
aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba, Dkt
Lutambi amesema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iko pamoja na wafiwa na watashiriki
mazishi kijiji cha Kowajese Mkoani wa Katavi.
|
Wananchi
waliojitokeza wakiaga mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP
Peter Charles Kakamba.
Na Mathias
Canal
Mwili wa
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi (SACP) EX Peter Kakamba umeagwa na wamia ya wakazi wa Mkoa wa Singida
wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Methew Mtigumwe.
Kakamba
alifariki dunia alfajiri ya tarehe 30/11/2016 katika hospital ya taifa
Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Kakamba
alizaliwa mwaka 1963 katika kijiji cha Kawajense Wilayani Mpanda, mkoa wa
Katavi. Alisoma shule ya msingi Shanwe Kawajense mwaka 1973 hadi 1980, Kidato cha kwanza hadi
cha nne katika shule ya Sekondari Kantalamba mwaka 1981 hadi 1984 ambapo kidato
cha tano na sita alisoma katika shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro
mwaka 1985 hadi 1987. Mwaka 1992 hadi 1994 alisoma Astashahada ya Sheria katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Marehemu
alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1988 ambapo katika utumishi wake
alipandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Konstable wa Polisi (1989), Sagenti wa
Polisi (1991), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1997), Mkaguzi wa Polisi (2003),
Mrakibu Msaidizi wa Polisi (2006), Mrakibu wa Polisi (2008), Mrakibu Mwandamizi
wa Polisi (2011), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2015) na Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi (2016).
Baadhi ya
nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa
Mwendesha Mashtaka wa Polisi katika mkoa wa Iringa, Mkuu wa Polisi wa
Wilaya ya Mufindi, Afisa mnadhimu wa Polisi katika Mikoa ya Iringa na Geita,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa na mpaka anafariki alikuwa Kamanda wa Polisi
katika mkoa wa Singida.
Kufuatia
kifo hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu anatoa pole kwa
Maofisa, Wakaguzi,Askari, ndugu, jamaa na marafiki kwa Msiba huo.
Bwana alitoa
na Bwana ametwaa,Jina la Bwana lihimidiwe - Amen.
|
No comments:
Post a Comment