|
Bondia
maarufu nchini Tanzania Francis Cheka, jana ametangaza rasmi kustaafu mchezo wa
msumbwi kwa kile alichokieleza ni ubabaishaji wa ma-promota pamoja na kutopata
faida katika mchezo huo.
Cheka ambaye
anakabiliwa na tuhuma za kuchukua pesa na kugoma kupanda ulingoni katika
pambano lililokuwa limeandaliwa siku ya Krismasi, amesema amechoshwa na kile
alichokiita kuwa ni utapeli wa mapromota, na kwamba sasa atajikita zaidi katika
mapambano ya kuhamasisha vijana.
Akiwa
amedumu kwenye ngumi nchini kwa
takribani miaka 19, Cheka amesema mchezo huo umetawaliwa na majungu, na fitina
huku watu wengi wakifikiri kuwa kuna pesa nyingi, wakati hakuna anachokipata
zaidi ya umaarufu na kuhojiwa kwenye vyombo vya habari.
"Huu mchezo una majungu na fitina, hakuna
faida yoyote zaidi ya kuhojiwa na waandishi wa habari, hakuna pesa, tunapata
pesa gani, watu wanadhani tunapata pesa,
nitabaki kucheza mapambano kwa ajili ya kuhamasisha vijana katika ngumi
pamoja na kufanya biashara nyingine nipate pesa, nimedumu kwenye ngumi zaidi ya
miaka 19, nimevumilia mengi" Alisema Cheka.
|
No comments:
Post a Comment