Sitta Azikwa Nyumbani Kwao URAMBO, TABORA. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, November 13, 2016

Sitta Azikwa Nyumbani Kwao URAMBO, TABORA.


Jeneza lenye likiandaliwa kushushwa kaburini kwa mashine maalum.

Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), Dk Alex Malasusa (mwenye kofia kushoto) akiwaongoza maaskofu, wachungaji, waumini na waombolezaji wakati wa ibada ya mazishi.

Viongozi wa serikali na vyama vya siasa, watoto wa marehemu, ndugu na marafiki wa marehemu wakiweka udongo kaburini.

Mjane wa Marehemu Sitta, Bi. Magreth Sitta akiweka shada kwenye kaburi la mumewe.

Aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta ,Novemba 12,2016 amezikwa mjini Urambo. Mazishi hayo yaliongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alitoa neno la faraja kwa wafiwa, marafiki na viongozi wa serikali. 

Mazishi hayo yalihudhuriwa na mawaziri, wabunge na wananchi mbalimbali wakiwemo wasanii wa filamu na muziki.

Aidha, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Elikael Mbowe naye alihudhuria na alikuwa mmoja wa viongozi waliotoa hotuba katika msiba huo.

Mara baada ya mwili wa marehemu kushushwa kaburini, viongozi mbalimbali wakiongozwa na waziri mkuu pamoja na wana familia waliweka mashada ya maua kwenye kaburi hilo kisha kikosi cha jeshi la polisi kilipiga risasi hewani kama heshima kwa kiongozi huyo aliyeaga dunia Novemba saba mwaka huu nchini Ujerumani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad