Mkuu wa mkoa
wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mstapha Kijuu.
Kamati ya
maafa ya mkoa wa Kagera iliyokuwa ikiendelea kupokea michango ya waathirika wa
tetemeko la ardhi, imeishapokea zaidi ya shilingi bilioni 5.4 hadi kufikia
Novemba 10 mwaka huu,2016.
Michango
hiyo ilikuwa ikitoka kwa wadau mbalimbali ambao ni pamoja na taasisi binafsi na
zile za kiserikali, mashirika ya kimaifa na nchi marafiki.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati akielezea juhudi za kamati hiyo katika
kukabiliana na madhara ya tetemeko, Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali
Mstaafu Salum Mustapha Kijuu, amesema kamati hiyo imeishatumia kiasi cha
shilingi bilioni 1.1 kutokana na michango hiyo kwa ajili kukarabati miundombinu
ambayo imeharibiwa ambayo ni pamoja na zahanati,vituo vya afya,shule za msingi
na sekondari.
Baadhi ya
viongozi wa serikali walikuwa wakifika mkoani humo wakiwasihi na kuwashauri
wakazi wa mkoa huo kuendeleza upya nyumba zao zilizoharibiwa na tetemeko hilo.
Mkuu wa mkoa alichukua nafasi kuwapongeza walioanza hatua hiyo.
“Nawapongeza
waliochukua hatua ya kujenga upya nyumba zao zilizoharibiwa na tetemeko. Kamati
ya maafa ya mkoa wa Kagera iko kwenye mchakato wa kuhakikisha makundi maalumu
yenye uhitaji yanarejeshwa katika hali ya kawaida miundombinu ya nyumba zao za
makazi yaliyoharibiwa na tetemeko,” alisema Kijuu.
“Kamati hiyo
tayari imeishafanya makubaliano na Kanisa la Pentekoste ambalo limeahidi
kujenga nyumba za wenye uhitaji kwa awamu mbalimbali ambapo katika awamu ya
kwanza kanisa hilo litajenga nyumba 370,”aliongeza.
Michango
hiyo ilikuwa ikipokelewa na waziri mkuu kwa kupitia akaunti maalumu ya maafa
mkoani Kagera.
|
No comments:
Post a Comment