Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa (wapili kulia) akimfariji mjane wa Spika Mstaafu Mama Margareth Sitta baada ya mwili wa Spika Mstaafu, Marehemu Samuel Sita kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimfariji mjane wa Spika Mstaafu Mama Margareth Sitta baada ya mwili wa Spika Mstaafu, Marehemu Samuel Sita kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai pamoja na viongozi wengine wakiusubiri mwili wa Spika mstaafu, Samuel Sitta uteremshwe kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa Dodoma Novemba 11, 2016
Mwili wa Spika Mstaafu Samuel Sitta ukiteremshwa kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Novemba 11, 2016.
Mwili wa Spika Mstaafu, Samuel Sitta ukiingizwa bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Mwili wa Spika Mstaafu, Samuel Sitta ukiingizwa bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Mwili wa Spika Mstaafu, Samuel Sitta ukiingizwa bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao maalum cha bunge cha kumuenzi Spika Mstaafu, Samuel Sitta, bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016.
Waziri Mkuu Mstaafu, Samuel Malecela akimpa pole mjane wa Spika Mstaafu, Margareth Sitta bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016.
1A2358 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye jeneza la Spika Mstaafu Samwel Sitta, bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Spika Mstaafu, Samuel Sitta, bungeni mjini Dodoma, Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameongoza mamia ya wabunge, viongozi wa kitaifa na watumishi wa
Ofisi ya Bunge kuuaga mwili wa Spika Mstaafu, Samwel Sitta.
Bw. Sitta
alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 7 katika hospitali ya Technical
University of Munich nchini Ujerumani.Akizungumza wakati wa kuuaga mwili huo Bungeni mjini Dodoma
leo (Ijumaa, Novemba 11, 2016), Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge,
Mheshimiwa Job Ndugai, mke wa marehemu Mheshimiwa Magreth Sitta, mama wa
marehemu Hajat Zuena Fundikila na familia ya marehemu na wabunge wote.
“Nitumie
fursa hii pia kukupa pole Mheshimiwa Spika kwa pigo ambalo Bunge lako tukufu
imelipata kwa kumpoteza mmoja wa viongozi mahiri wa Bunge hili katika historia
ya nchi yetu. Msiba uliotupata wa Spika Mstaafu wa Bunge la Tisa (2005-2010) na
Mbunge Mstaafu wa jimbo la Urambo mkoani Tabora ni mzito.”
Amesema Bw.
Sitta alikuwa mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi na
maendeleo. “Serikali imepokea taarifa za
msiba huu kwa mshtuko mkubwa. Historia ya Mzee Sitta ni pana sana. Tunatambua
utumishi uliotukuka katika nyadhifa mbalimbali alizozitumikia. Tutamkumbuka kwa
utumishi wake,” amesema.
Waziri Mkuu
ameongeza kuwa: “Tuzidi kumuomba Mwenyezi Mungu kila mtu kwa imani yake ili
tuweze kufikia japo mema machache aliyoyatenda katika enzi za uhai wake.”
Enzi za uhai
wake Mhe. Sitta alibahatika kufanya kazi na Marais wa awamu nne zilizopita
tangu ya kwanza ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, akiwa mbunge
kwa miaka 30.
Nyadhifa
nyingine alizowahi kushika ni pamoja na Mkuu wa Mikoa ya Iringa na Kilimanjaro,
Waziri wa Ujenzi, Waziri anayesimamia Ustawishaji Makao Makuu, Waziri wa Katiba
na Sheria, Waziri wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba.
No comments:
Post a Comment