Kagera Sugar U20 waanza kwa Sare Leo November 15, 2016 dhidi ya Yanga SC U20. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, November 15, 2016

Kagera Sugar U20 waanza kwa Sare Leo November 15, 2016 dhidi ya Yanga SC U20.

Ligi ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20  kwa klabu zote za Ligi Kuu ya Vodacom imeanza rasmi leo Novemba 15, 2016 kwa mchezo maalumu wa ufunguzi uliofanyika Uwanja wa Kaitaba, Mjini Bukoba mkoani Kagera.

 Kituo hicho cha  Bukoba mkoani Kagera ambako kuna timu za Azam FC, African Lyon, Mbao FC, Toto Africans, Mwadui FC ya Shinyanga kama ilivyo Stand United, -Timu ya Kagera Sugar na Young Africans  zimefungua dimba kwa mchezo pekee katika uwanja wa kaitaba uliyopo  Manispaa ya  Bukoba ambapo timu hizo zimemaliza dk 90  kwa kutoshana nguvu ya goli 1-1 .

Bao la Yanga SC U20 lilifungwa dakika ya 69 kipindi cha pili.


Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)-Vituo vilivyopangwa ni Dar es Salaan ambako kuna timu za JKT Ruvu, Simba SC, Ruvu Shooting, Ndanda FC, Majimaji FC ya Songea, Mtibwa Sugar, Mbeya City na Tanzania Prisons.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad