Bi.Alfreda Ndungulu
Mkuu wa Chuo cha Uuguzi , Wilayani Kibondo mkoani Kigoma.
Akiongea katika
mahafali ya saba kwa wahitimu ngazi ya
cheti ,Jana September 05,2016, Mkuu wa chuo hicho Bi. Alfreda Ndungulu alisema
licha ya walimu kujituma kufanya kazi kwa bidii lakini changamoto hizo zimekuwa
zikiwalemea kwa kukosa mahitaji muhimu kama vifaa vya maabara kwa ajili ya
kufundishia huku akiiomba serikali kupitia wizara ya Afya maendeleo ya Jamii Jinsia,
Wazee na Watoto kulitazama kwa namna ya pekee.
Nao
wanafunzi waliokuwa wakihitimu kwenye chuo hicho cha uuguzi ambao ni Adela
James na Mary Esau, walisema ni vema
serikali ikaweka mpango wa kuwakopesha wanafunzi katika sekta ya Afya kwa ni nayo ni muhimu huku wakieleza hali
waliyokuwa wakikumbana nayo wakati wa masomo yao walikuwa wakitegemeaf edha
kutoka kwa wazazi ambazo zilikuwa hazikidhi mahitaji na kulazimika kula mlo mmoja kwa sikua Adela.
‘’Jinsi
ambavyo mikopo inatolewa na serikali basin a sisi tungewekewa utaratibu wa
kupata mikopo kwa tunapata shida sana kwa kutegemea fedha za wazazi
ikilinganishwa hata huduma za afya ni muhimu kwani hata masomo yake lazima uwe
umetulia ili kupata uelewa mzuri wakati wa masomo bila kuwa mawazo ya Ada na
mahitaji mengine alisema Adela.
|
No comments:
Post a Comment