Picha 13 za Lori laanguka katika mlima wa K9 wilayani Ngara/Kagera na kuua Mtu mmoja. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, September 02, 2016

Picha 13 za Lori laanguka katika mlima wa K9 wilayani Ngara/Kagera na kuua Mtu mmoja.

Mtu mmoja  raia wa nchini Uganda amefariki dunia  na mwingine kujeruhiwa baada ya kupata ajali ya agari katika kijiji cha Kasharazi  wilayani Ngara mkoani Kagera ambapo gari walilokuwa wakisafiria kupoteza mfumo wa breki na kupinduka.

Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Ngara Abel Maige amemtaja raia huyo kuwa ni Peter Kyalo mwenye umri wa miaka 30 na kwamba ajali hiyo imetokea jana Septemba 01,2016  na kwamba aliyejeruhiwa ni utingo wa agari hilo Bw  Semaganda Ally, (21) ambaye amejeruhiwa mguu na mamelazwa hospitali ya Nyamiaga wilayani Ngara.





Maige amesema gari lililopinduka ni  aina ya Scania lenye namba za usajili KCA 664U/ ze 9024a m/benz mali ya kampuni ya primehauliers E.A ltd ambalo lilikuwa limepakia rola za kutengenezea mabati kutoka nchini kenya kwenda Burundi.

Hata hivyo baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo katika mlima wa k9 wamesema baada ya ajali hiyo kutokea askari wa JWTZ kikosi cha K9 kwa kushirikiana na wananchi waliweza kuutoa mwili wa marehemu chini ya gari ambalo lilipinduka mbele ya lile lililopata  ajali Jumatatu,Agosti 29,2016 na Watu watatu kufariki papo hapo.







 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad