The Registered Trustee of Chemchem
Trust Wakitoa Msaada wao wa Cementi Mifuka 600 kwa Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe, Meja Jenerali Mstaafu Salim M. Kijuu ambaye ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya mkoa.
|
Jumuiya Wazazi CCM Taifa Mara Baada ya Kutoa Msaada Wao. |
Kagera Tea Company Ltd Wakitoa Mbao
250.
|
Kanisa la Pentecostal Wakitoa Msaada Wao kwa Mhe Kijuu. |
Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu Akiongoza
Zoezi la Kugawa Mahitaji kwa Wahanga wa tetemeko la ardhi la Kagera September 10,2016
jana September 14, jioni.
|
JIEPIGO kwa Ufadhili wa
Watu wa Marekani Wakitoa Msaada wa Vifaa Tiba na Dawa .
|
Serikali ya Mkoa wa
Kagera , Septemba 14, 2016 tayari imepokea misaada mbalimabli ya fedha
taslimu na mahitaji mbalimbali kama Sukari, Mchele, Unga, Maji ya kunywa,
Sabuni, Blanketi, Shuka Maharage, matrubali, Mbao na Sementi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni
32.
Aidha, Kamati ya Maafa
ya Mkoa tayari imeanza kugawa mahitaji hayo kwa wananchi waliopatwa na janga la
tetemeko na kwa sasa hawana mahala pa kuishi.
Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa
Kashabo Manispaa ya Bukoba wamegawiwa mahita ji hayo na aliyeongo zoezi hilo ni
Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe, Meja Jenerali Mstaafu Salim M. Kijuu ambaye ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya mkoa.
Katika hatua nyingine
Kamati ya Maafa ua Mkoa imeamua kutoa bati 20 na sementi mifuko 5 kwa kila
mwananchi ambaye nyumba yake ilianguka kabisa au haifai kuishi tena. Aidha, wapangaji waliokuwa wanapanga katika
nyumba hizo watalipiwa kodi ya miezi na Serikali sita kila mwezi 20,000/=
Katika hatua nyingine
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu ameandaa kikao cha harambee ya kuchangia
maafa mkoani Kagera tarehe 16.09.2016 siku ya Ijumaa katika ukumbi wa Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa kuanzia saa 3:00 Asubuhi na
anawaalika wadau wote kuja kuchangia katika harambee hiyo.
Aidha kwa wale
wanaotaka kuchangia lakini hawatahudhuria wanaweza kuchangia kupitia Akaunti ya
Benki iliyopo CRDB inayojulikana kama “KAMATI YA MAAFA KAGERA CRDB BUKOBA”
Akaunti Namba. 0152225617300. Tunawashukuru wote wanaoendelea kuchangia na
Mungu awazidishie.
Imetolewa na: Sylvester
M. Raphael
Afisa
Habari (Mkoa )
KAGERA
Septemba 14,2016
No comments:
Post a Comment