Mabalozi na Wafanyabiashara Wachangia Waathirika Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, September 14, 2016

Mabalozi na Wafanyabiashara Wachangia Waathirika Kagera.

Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa  akipokea hundi ya shilingi milioni 100 kutoka kwa Charge d’ Affairs wa ubalozi wa China nchini, Bw. Haodong Gou  wakati alipokutana na wafanyabiashara na mabalozi wa nchi mbalimbali hapa nchini na kuwaomba wasaidie kuchangia ujenzi na ukarabati wa miundombinu iliyoathiriwa na tetemeko laardhi mkoani Kagera. 

Mkutano huo ulifanyika Ikulu jijini Dar es salaam Septemba 13, 2016.Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Suzan Kolimba. 

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri  MKuu wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa  ameongoza harambe maalum iliyofanyika jijini Dar es Saalm ikiwakutanisha mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, umoja wa wafanyabiashara na mtu mmoja mmoja aliyeguswa na tukio la tetemeko la ardhi mkoani Kagera lililopelekea maafa makubwa yakiwamo mauaji na uharibifu wa miundombinu.

Kwenye harambe hiyo iliyoudhuriwa pia na Waziri wa viwanda na biashara, Mhe. Charles Mwijage jumla ya pesa zilizochangwa ni shilingi za kitanzania 1,396,000,000/=.

Pesa hizo taslimu na ahadi zilizotolewa na wageni mbalimbali waalikwa. Ambapo zimetolewa katika mafungu yafuatayo milioni 700, milioni 600, Euro 10,000 na Dola 10,000 na kufanya jumla yake kuwa 1,396,000,000/= kwa pesa za Tanzania.

Pia wafanyabiashara wakubwa wa makampuni matatu tofauti wameungana na kuahidi kukamilisha ukarabati wa shule za sekondari za Ihungo na Nyakato ndani ya siku thelathini kuanzia leo, makampuni hayo ni Oil Com, GPP na Moyo Group.

Baadhi ya wafanyabiashara waliochangia michango yao ni pamoja na Regnald Mengi (Milioni 110), umoja wa wauza mafuta ya rejereja (Milioni 250), Kiwanda cha sukari  Kagera (Milioni 100), IPTL (Milioni 100), China (Milioni 100) Dewji Foundation (Milioni 100), Mambo ya Nje (Milioni 10), Azania (Milioni 20).

Jumla ya fedha na ahadi zilizotolewa kuwasaidia waathirika tetemeko la ardhi ni takribani Sh1.4 bilioni pamoja na vifaa vya ujenzi.

Tetemeko hilo lililotekea Septemba 10,2016.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad