
Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa wito kwa
wananchi kushirikiana na wataalam wanaofanya Mapitio ya Sera ya Afya
kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Chuo cha Afya Muhimbili na Wataalam
wa Ofisi mbalimbali za Serikali zinazojishughulisha na masuala ya
utekelezaji wa Sera ya Afya ya mwaka 2007.
************************************************
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TAARIFA KWA UMMA
MAPITIO YA SERA YA AFYA YA MWAKA 2007
Utoaji wa huduma za afya nchini una simamiwa na Sera ya Afya ya mwaka
2007.
Dhumuni kuu la Sera hii ya Afya ya Mwaka2007, ni kuinua hali ya
afya ya wananchi wote na hasa wale walioko kwenye hatari zaidi, kwa
kuweka mfumo wa huduma za Afya utakaokidhi mahitaji ya wananchi na
kuongeza umri wa kuishi wa Watanzania.
Mpaka sasa, Wizara yangu
inaendelea kutekeleza Sera hii katika kusimamia utoaji na upatikanaji wa
huduma za afya nchini.
Katika utekelezaji wa Sera hii, Wizara na Sekta
ya Afya kwa ujumla imepata mafanikio mbalimbali.
Mafanikio haya ni
pamoja na:
Ongezeko la Vituo vya kutolea Huduma:
Wizara imeendelea kuboresha
huduma za tiba kwa kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi
(MMAM).
Katika utekelezaji wa Mpango huo,vituo vya kutolea huduma za
afya vimeongezeka kutoka vituo 5,172 mwaka 2005 hadi 7,247 mwaka 2015,
sawa na ongezeko la vituo 2,075. Kati ya vituo vyote vilivyopo nchini,
Vituo 5,072 ni vya Serikali na 2,175 nivyataasisibinafsi.
Kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutoka112 kwa kila
vizazi hai 1000 mwaka 2005 hadi 81 kwa vizazi hai 1000 mwaka 2010.
Aidha, Taarifa ya Kimataifa ya Septemba 2013, imeonesha kuwa Tanzania
tumeweza kufikia Lengo la millennia namba 5, la angalau kuwa na vifo 54
kwa kila vizazi hai 1000, Tanzania iliweza kufikia lengo hilo kabla ya
mwaka 2015.
VifovitokanavyonamatatizoyaUzazivimepunguakutoka 578 kwakilavizazihai
100,000 mwaka 2005 hadivifo 432 kwavizazihai 100,000 mwaka 2012 navifo
410 kwavizazihai 100,000 mwaka 2014.
Pia matumiziyaUzaziwampangoyameongezekakutokaasilimia 20 mwaka 2005
hadiasilimia 27 mwaka 2010.
Huduma za Chanjo:
Serikali imefanikiwa katika kupanua wigo wa huduma
za chanjo ambapo,kiwango cha chanjo kimeongezeka kutoka asilimia 90
mwaka 2005 hadi asilimia 97 mwaka 2014.
Kutokana na mafanikio katika
chanjo, Wizara imefikia viwango vya kimataifa vya kutokomeza pepopunda
kwa watoto wachanga mwaka 2012 na pia imeweza kudhibiti ugonjwa wa
Polio.
Katika kipindi hiki cha kutekeleza sera hii, Wizara imeanzisha huduma
mpya za kibingwa na uchunguzi hapa nchini na kuwawezesha wananchi
kupata huduma za kibingwa ambazo awali zilikuwa hazitolewi hapa nchini.
Huduma hizo ni pamoja na upasuaji mkubwa wa moyo, upasuaji wa
mifupa,mishipa ya fahamu na ubongo, kusafisha damu kwa wagonjwa wenye
matatizo ya figo na uanzishaji wa huduma za dharura.
Udhibiti wa Malaria:
kiwango cha maambukizi ya malaria kimeshuka
kutoka asilimia 18 mwaka 2008 na kufikia asilimia 10 mwaka 2012
(THMIS).
Udhibiti wa UKIMWI:
Serikali imepata mafanikio katika kudhibiti
UKIMWI, kiwango cha maambukizi ya Virusi vya UKIMWI(VVU) kimepungua
kutoka asilimia 7 mwaka 2004 hadi kufikia asilimia 5.1 mwaka 2011/12.
Vituo vya tiba kwa watu wanaoishi na VVU vimeongezeka kutoka 91 mwaka
2005 hadi 1,463 mwaka 2015. Hadi Juni 2015, jumla ya watu 703,589
wanapatiwa ARV ikilinganishwa na Mwaka 2005, ambapo watu wanaoishi na
VVU 16,199 walipatiwa huduma hii.
Pamoja mafanikio mbalimbali yaliyopatika katika utekelezaji wa Sera
hii, Sekta ya Afya imekuwa na changamoto mbalimbali na kusababisha
madhumuni ya Sera kutofikiwa.
Changamoto hizo ni pamoja na:
Upungufu wa vifaa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na dawa katika vituo vya kutolea huduma za Afya, Uhaba wa miundombinu ya kutolea huduma za afya nchini hasa, zahanati, vituo vya afya na hospitali, Uwezo mdogo wa viwanda vinavyozalisha dawa hapa nchini,
Upungufu mkubwa wa watumishi wa Afya katika ngazi zote za kutolea huduma
Maendeleo madogo ya upunguzaji wa Vifo vya wakinamama vinavyotokana na Ujauzito.
Maendeleo na mabadiliko ya tabia na mwenendo wa maisha vimebadili
sura ya magonjwa. Aidha, hali hii imesababisha kuanza kujitokeza kwa
magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza na yanayotokana na ajali
na majanga, ambayo kwa huduma zilizopo haziwezi kukidhi.
Kuendelea kupungua kwa Rasilimali fedha katika Sekta ya Afya na
kusababisha kuendelea kushuka kwa ubora wa huduma za afya katika vituo
vya kutolea huduma.
Kuwalinda wananchi hasa wenye kipato cha chini katika katika kupata huduma za afya wakati wanazihitaji.
Uwepo wa vituo vya kutosha vya kutolea huduma na kudumisha upatikanaji wa huduma bora za afya katika vituo vya afya.
Ongezeko la idadi ya watu ambalo linapelekea ongezeko la mahitaji ya huduma za afya.
Aidha, changamoto hizo na Mabadiliko mbalimbali ambayo yatatokea
yamepelekea serikali kutoa maagizo na kutayarisha mikakati mbali mbali
ya Serikali kwa lengo la kuboresha huduma zitolewazo kwa umma.
Mikakati
na maagizo hayo ni pamoja:
Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Nne wa Sekta ya Afya 2015-2020 ( HSSP IV) Utekelezaji wa Mkakati wa Ugharamiaji wa Huduma za Afya
Utekelezaji katika mfumo wa malipo kwa matokeo.
Mpango wa Serikali wa matokeo makubwa sasa
Mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia, inayobadilisha namna huduma za Afya zinavyotolewa Ongezeko la Magonjwa sugu, hasa magonjwa ambayo siyo ya kuambukiza ambayo yana gharama kubwa na yanaweza kuzuilika.
Kutokana na changamoto zilizojitokeza na utekelezaji wa mikakati na
maagizo hayo , ni muhimu kufanya mapitio ya Sera ya Afya ya mwaka 2007
ili utekelezaji wa matamko ya kukidhi Lengo na Madhumuni
yaliyokusudiwa kufikiwa na Sera.
Mapitio haya, yanafanywa na Wizara yangu kwa kushirikiana na Chuo
kikuu cha Dar es Salaam, Chuo cha Afya Muhimbili na Wataalam wa Ofisi
mbalimbali za Serikali zinazojishughulisha na masuala ya utekelezaji wa
Sera ya Afya ya mwaka 2007.
Nawaomba wananchi wote kutoa ushirikiano wakutosha kwa Wizara na
Wataalam wa timu hii katika kuhakikisha kuwa mnatoa maoni yenu kwa uwazi
kwa ajili ya kusaidia maendeleo a Sekta ya Afya nchini.
Wananchi wote mnaweza kutoa maoni yenu kupiti Tovuti ya Wizara (www.moh.go.tz) au kuwasilisha maoni yenu pia Kupitia anuanimaoni.sera@moh.go.tz. Mwisho wa kutoa maoni ni tarehe 30 Oktoba 2016.
Nawashukuru sana.
Ummy A. Mwalimu (mb)
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto






No comments:
Post a Comment