![]() |
|
Waziri Nape
akizungumza kabla ya kukabidhiwa uwanja huo Agosti 22, 2016. Kulia ni Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Elisante Ole Gabriel, na kushoto ni mshauri wa
ujenzi, Injinia Aloyce Peter Mushi (PICHA NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID)
|
![]() |
|
Waziri Nape,
(wapili kushoto), Katibu Mkuu Profesa Ole Gabriel, (wakwanza kushoto),Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo, Alex Makoye Nkenyenge, (watatu
kushoto) na Injinia Mushi, wakikagua uwanja huo.
|
![]() |
|
Waziri Nape,
akikagua nyasi bandia uwanjani.
Akitoa
taarifa ya ujezni huo, mshauri huyo mwelekezi wa ujenzi, Injinia Aloyce Peter
Mushi alisema, uwanja huo una uwezo wa kuchukua watu milioni 22 na ulikamilika
na kuanza kutumika kwa mara ya kwanza Mei 22, 2015.
Naye Meneja
Mkuu wa Kampuni ya BCAG, Cheng Long Hai, alisema, uwanja huo umewekewa mifumo
yote muhimu kama vile tangi la kuhifadhia maji na mifumo ya maji taka, na
kuishukuru serikaliya Tanzania kwa kuiaminikampuni yake kutekeleza mradi huo
mkubwa.
|
![]() |
|
Alama ya
uwanja wa Uhuru ni jukwaa hili kuu, kama linavyoonekana leo Agosti 22, 2016.
|
![]() |
|
Vyoo vya
kisasa, (kushoto) wanawakena kulia wanaume.
Naye Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel,
alisema, amekuwa akipokea maombi mbalimbali ya wanamichezo na watu wengine
kuomba kuutumia uwanja huo na kuwahakikishia kuwa utaratibu unapangwa ili
watanzania waanze kufaidi matunda ya uwanja huo ambao kutokana na ukongwe wake
ulipachikwa jina la shamba la bibi.
“Nitoe rai
tu kwa watanzania, leohii Agosti 22, 2016 ambapo tumekabidhiwa uwanja huu rasmi
ukiwa umekamilika, naomba hilo jina la shambala bibi nalo lifikie kikomo kwani
uwanja huu sa sa unauonekano mpya na wa kisasa.” Alisema Profesa Gabriel.
Ukarabati
huo mkubwa ulihusisha ujenzi wa jukwaa na paa, ikiwa ni pamoja na miundombinu
mingine ya uwanja kama vile, mifumo ya kusambaza maji, na kutoa maji taka,
uwekani wa tanki la kuhifadhia maji, pamoja na ujenzi wa vyoo vya kutosha
uwanjani...PICHA ZAIDI GONGA HAPA
|











No comments:
Post a Comment