|
Wakimbizi
waliopewa uraia wameendelea kuingiza ndugu zao. Naagiza kamati ya ulinzi na
usalama ya mkoa ifanye ukaguzi katika kambi zote kwa sababu zimegeuzwa kuwa
maficho ya kuwahifadhi watu wanaoingia nchini bila ya vibali,” alisema.
“Hakikisheni
mnachukua hatua kwa wote watakaoingiza watu kinyemela katika kambi za wakimbizi
za Mishamo na Katumba.
Pia msiruhusu watu kuleta silaha kwenye maeneo haya.
Tanzania watu wanaoruhusiwa kutembea na silaha ni askari tu,” alisisitiza.
Waziri Mkuu
alisema lazima ulinzi uimarishwe katika maeneo ya mipakani na wasipofanya hivyo
watu wengi wataingia nchini bila ya kuwa na vibali hivyo kusababisha ongezeko
kubwa la idadi ya watu.
Wakati huo
huo Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda wasiwaudhi
wakulima na wafanyabiashara wadogo kwa kuwatoza ushuru kwenye mazao wanapotoka shambani kama debe
moja la nafaka na wanaouza bidhaa ndogo ndogo.
“Mkulima
ametoka shambani na debe moja la mahindi unamtoza ushuru maana yake nini?
Halmashauri tusitafute mgogoro katika hili. Tafuteni biashara za kutoza ushuru,
mkulima anatoka kijiji cha Kanoge anakwenda kijiji cha Ikongo ushuru wa
nini?" Waziri Mkuu alihoji.
Waziri Mkuu
alisema “Tumewasisitiza mkusanye kodi lakini siyo hivyo. Mkiendelea kutoza
ushuru kwa wakulima wanaotoka shambani na mahindi kidogo mtasababisha wakate
tamaa ya kulima,”.
|
No comments:
Post a Comment