![]() |
|
Mbunge wa
Geita Mjini Mh. Constantine John Kinyasu akitoa maelezo kwa watendaji wa
hospitali ya Mkoa wa Geita.
|
![]() |
|
Baadhi ya
wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya
Dk. Kigwangalla (hayupo pichani).
Naibu Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi
Kigwangalla ametoa maagizo mazito kwa watendaji wa Wizara hiyo kesho tarehe 22
Agosti.2016 kuhakikisha wanamfikishia taarifa ya kina kuhusu upungufu wa chanjo
nchini.
Akiwa ziara
ya kikazi Mkoani Geita, Ameagiza akute maelezo ya kina mezani kwake, kuwa ni
nani haswa amesababisha chanjo kupungua kwenye maeneo mengi nchini? Na mpaka
sasa amechukuwa hatua gani za kuwajibika?
Je,
changamoto ipo hazina ama kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa Huduma za kinga?
“Vyovyote vile, nataka utetezi uje ukiwa na vielelezo, kabla sijachukua hatua
stahiki. Chanjo ni eneo pekee kwenye sekta ya Afya tulilofanikiwa kwa zaidi ya
95%! Haikubaliki kurudisha nyuma mafanikio haya."
Alisema,
Baadhi ya maeneo chanjo zipo na wana dozi za mwisho na baadhi hazipo kabisa.
Mfano bohari ya chanjo Mkoa wa Geita hakuna chanjo za OPV, Rotavirus, BCG na
Tetanus. Wangepaswa kuwa na akiba ya miezi mitatu mbele.
Kwenye ngazi ya Taifa
wanapaswa kuwa Na chanjo za miezi Sita mbele, hapo ndipo tunaweza kusema tuna
chanjo za kutosha.Kwa
picha zaidi BOFYA HAPA
|








No comments:
Post a Comment